TBS YAWATAKA WAHANDIS,WAKANDARASI NA WADAU KUDHIBITISHA UBORA WA BIDHAA

 

Mkurugenzi wa upimaji na ujenzi wa TBS, Mhandisi Johanes Maganga,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye bando ambapo wameshirika kwenye maonyesho ya Mkutano wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano unaofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili.

Afisa Viwango,Projestus Kasimbazi,akitoa elimu kwa mshiriki aliyetembelea bando la TBS katika maonyesho ya Mkutano wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano unaofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili.

……………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Shirika la viwango Tanzania (TBS) limewataka wahandisi, wakandarasi na wadau wa sekta ya ujenzi kununua na kuthibitisha ubora wa bidhaa zao kwa kutumia shirika hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa upimaji na ujenzi wa TBS, mhandisi Johanes Maganga, amesema ili kupata bidhaa bora zenye viwango vinavyokidhi mahitaji, wadau wa sekta hiyo wasihofu kulitumia shirika hilo kwakuwa ndilo lenye dhamana na linatimiza jukumu lake kwa weledi.
“Moja ya kazi tunazozifanya ni kudhibiti ubora wa vifaa vinavyotumika kwenye sekta ya ujenzi, iwe ni vile vinavyotengenezwa ndani au vinavyotoka nje ya nchi” Alisema mhandisi Maganga.
“Kwa vifaa vinavyotengenezwa ndani huwa tunachukua sampuli toka sokoni au bandarini na kuzipima, lakini kwa vile vinavyotoka nje tunao mawakala wanaofanya kazi hiyo na kutoa vyeti” Aliongeza mhandisi Maganga.
Mhandisi Maganga amefafanua kuwa shirika hilo hutoa leseni za ubora kwa bidhaa zilizohakikiwa na kuthibitishwa kwamba ubora wake umefikia viwango vilivyowekwa.
Shirika la viwango nchini TBS, ni taasisi ya serikali yenye mamlaka ya kisheria kudhibiti na kuthibitisha ubora wa bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa ndani au nje ya Tanzania kabla ya kuingia sokoni na kutoa cheti cha ubora kinachotoa uhakika wa ubora kwa watumiaji wa bidhaa husika

Post a Comment

Previous Post Next Post