Leo tarehe 22 Septemba, 2020 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina ametembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Kiwanja cha Kituo cha Uwekezaji Cha Bomba Mbili mjini Geita.
Mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalam, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Tume ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini.
Aidha amepongeza kasi ya utoaji wa leseni ndogo za madini kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kuongeza kuwa mafanikio ya Tume ya Madini yanaonekana kwa sasa.