DKT.NZUKI: MRADI WA REGROW UTACHOCHEA UTALII UKANDA WA KUSINI

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki (kulia) akifungua Kikao cha Kamati tendaji ya Mradi wa Regrow kilichofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Mkoani Morogoro. Kulia ni Mraitibu wa Mradi wa Regrow Bw. Aenea Saanya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Mradi wa Regrow Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bi. Zena A. Said (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utali Dkt. Allan Kijazi (kulia) pamoja na wajumbe wa kamati Tendaji ya Mradi wa Regrow mara baada ya Kikao cha kamati kilichofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Mwenyekiti wa Kamati tendaji ya Mradi wa Regrow Dkt. Aloyce K. Nzuki akieleza mambo muhimu ya kuzingatia katika utekelezaji wa Mradi wa Regrow wakati wa Kikao cha Kamati tendaji ya Mradi huo kilichofanyika katika ukumbi mdogo uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, mkoani Morogoro. Kushoto mwandike ni Mratibu wa Mradi wa Regrow Bw. Aenea Saanya.

Karibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bi. Zena A. Said akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati Tendaji ya Regrow kilichofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utali Dkt. Allan Kijazi (kushoto) akisoma agenda mbalimbali za kikao cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Regrow wakati wa Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi katika wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
……………………………………………………………….
Na. JohnI. bera,MOROGORO.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Aloyce K. Nzuki amesema mradi wa Regrow utasaidia kuendeleza maliasili na kukuza utalii katika ukanda wa Kusini katika Hifadhi za kipaumbele ambazo ni Ruaha,Udzungwa na Mikumi

Aidha, Amesema mradi huo utasaidia kuchagiza uchumi wa Wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi hizo kwa kuwawezesha kushiriki moja kwa moja katika shughuli za utalii.

Akizungumza katika Kikao cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Regrow kilichofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Dkt.Nzuki amesema ujio wa mradi huo utachochea kukua kwa shughuli za utalii katika ukanda huo ambao umekuwa nyuma kwa muda mrefu kwa kutokana na ubovu wa miundombinu.

Amesema katika katika kuhakikisha shughuli za utalii zinakua na kuendelezwa katika ukanda wa Kusini, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango iliamua kuomba mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia utakaowezesha kuboresha miundombinu katika Ukanda wa Kusini.

Amesema msingi wa maamuzi hayo ulitokana na ukosefu wa miundombinu iliyo bora ya kuvutia uwekezaji katika sekta ya utalii. Hivyo, Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine wa uhifadhi pamoja na Benki Dunia walianza mchakato wa majadiliano.

Akizungumzia faida za mradi huo, Dkt.Nzuki amesema Serikali itaweza kuongeza uwezo kuhifadhi rasilimali za wanyamapori ambazo ndio uti wa mgongo wa utalii wa Tanzania.

Mbali faida hiyo, Dkt.Nzuki amesema idadi ya watalii itaongezeka ukilinganisha na idadi ya watalii wanaotembelea vivutio vya utalii vya Kusini kwa sasa hali itakayochochea ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu, Dkt.Nzuki amesema licha ya mradi huo kuchelewa kuanza kutekelezwa lakini umeanza kuonesha mafanikio ambapo hadi kufikia Agosti mwaka huu umefanya manunuzi makubwa ya vifaa vya doria ambavyo tayari vimeanza kutumika katika Hifadhi za Ruaha,Mikumi na Udzungwa. Mafanikio mengine ni ununuzi wa mitambo ya mindombinu mbalimbali, ununuzi wa magari 14 kati ya 23 na mengine 18 yatawasili kati ya mwezi Septemba na Novemba mwaka huu.

Post a Comment

Previous Post Next Post