DC KINONDONI ARIDHISHWA NA KASI YA DAWASA YA KUPELEKA HUDUMA YA MAJI KWA WANANCHI

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo ameridhishwa hatua zinazofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) za kupeleka miradi mbalimbali ya Maji  inayoendelea kutekelezwa Wilaya ya Kinondoni.


Akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa maji unaonzia Chuo kikuu cha Dar es Salaam hadi Bagamoyo ,akiwa eneo la Mabwepande, Chongolo amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo hususan ulazaji wa miundombinu ya Maji na kuwahakikishia wananchi wa  Jimbo la Kinondoni kufikiwa na Maji kwa asilimia 100.

DC Chongolo amesema tayari Mtandao wa Maji umeanza kujengwa wenye urefu wa Km 1219 ambao unalenga kusambaza Maji katika maeneo ya Mabwepande, Mivumoni, Mbopo, Madale, Nyakasagwe, Tegeta A, Goba ,Wazo Hill, Chuo Kikuu, Ardhi na maeneo ya Makongo Juu.

"Nimeridhika na kazi inayoendelea hapa, jitihada zinaonekana na matokeo tunayaona, tumeona mabomba yamesambazwa sehemu mbalimbali naamini muda mfupi ujao Wananchi watafurahia huduma ya Maji na kurahisha shughuli mbalimbali", amesema Chongolo.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi huo wa Maji kutoka DAWASA, Mhandisi Ishengoma Kakwezi amesema Mamlaka  inafuata maelekezo ya Serikali na  kuhakikisha 
Msimamizi wa Mradi wa Maji kutoka DAWASA, Mhandisi Ishengoma Kakwezi(wa tatu kushoto) akimuonesha kwenye ramani  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo(wa pili kushoto) kuhusu DAWASA walivyofanikiwa kutandika mabomba katika eneo la Mabwepande wakati wa ziara ya yake ya kutembelea mradi wa maji unaonzia Chuo kikuu cha Dar es Salaam hadi Bagamoyo .Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) (DAWASA) Neli Msuya.
Mkandarasi Mshauri kutoka Nicholas O'dwyer,  Seveline Alfred akitoa ufafanuzi kuhusu mradi unaotekelezwa na DAWASA wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo ya kutembelea mradi wa maji unaonzia Chuo kikuu cha Dar es Salaam hadi Bagamoyo.
Mkandarasi Mshauri kutoka Nicholas O'dwyer,  Seveline Alfred akitoa ufafanuzi kuhusu namna walivyolaza mabomba ya ichi 3 katika eneo la Mabwepande wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo ya kutembelea mradi wa maji unaonzia Chuo kikuu cha Dar es Salaam hadi Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akifukia bomba mara baada ya kumalizika utandikwaji wa mabomba hayo ya kusambazia yenye  upenyo wa inchi 3 maji ya DAWASA wakati wa  kutembelea mradi wa maji unaonzia Chuo kikuu cha Dar hadi Bagamoyo.
Msimamizi wa Mradi wa Maji kutoka DAWASA, Mhandisi Ishengoma Kakwezi akitoa ufafanuzi kuhusu tenki la kuhifadhia maji namna litakavyoweza kuhudumia mitaa mbalimbali ya Wilaya ya Kinondoni wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo alipotembelea  mradi wa maji unaonzia Chuo kikuu cha Dar hadi Bagamoyo, ikiwa miradi hii itatekelezwa na DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo  akitoa pongezi kwa DAWASA kwa kuendelea kujenga miundombinu ya maji hasa tenki lililopo katika kata ya Mabwepande litakaloweza kuhudumia maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo. 
Msimamizi wa Mradi wa Maji kutoka DAWASA, Mhandisi Ishengoma Kakwezi akitoa utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa maji katika Mtaa wa Mabwepande mara baada mkuu wa wilaya hiyo ya kutembelea mradi wa maji unaonzia Chuo kikuu cha Dar es Salaam hadi Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza na watendaji wa mtaa wa Mabwepande mara baada ya kufanya ziara ya kukagua mradi wa utandikaji wa mabomba ya kusambazia yenye  upenyo wa inchi 3 na robo ya kupitishia maji ya DAWASA wakati wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa maji katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Zoezi la utandikaji wa mabomba ya kusambazia yenye  upenyo wa inchi 3 na  na robo ya kupitishia maji ya DAWASA ukiendelea katika eneo la Mabwepande 
Baadhi ya mabomba yatakayotumika kutandikwa katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Mabwepande yakiwa kwenye mradi huo
Kazi ikiendelea ya kufunika mambomba

Post a Comment

Previous Post Next Post