Waziri Mpina Aridhishwa Na Uzalishaji Wa Maziwa Katika Kiwanda Cha Galaxy Jijini Arusha.

 


 Pichana Ujumbe uliongozana na Waziri ukikagua baadhi ya shughuli kiwandani hapo
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akisikiliza maelekezo kutoka kwa Hasheem Said ambaye ni Muendeshaji (Operator) katika Kiwanda Cha Galaxy Food and Beverage limited.

 Maziwa Aina ya mtindi Maarufu Kama Kilimanjaro fresh Mtindi yakiwa katika hatua za Mwisho kupelekaa kwa mlaji.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga  Mpina amekiagiza kiwanda cha Galaxy Food and Beverage limited kuhakikisha kuwa kinathibiti Viwango vya Bei ya Maziwa ili kuondoa hujma za kiabiashara ambazo zinaweza kufanywa ili kushusha thamani ya Maziwa ambayo yanayozalishwa hapa nchini.

Mpina alisema kuwa mifumo ya Bei inapaswa kuangaliwa kwa Ukaribu Sana kwa kuwa Maziwa yanaweza kuuzwa kwa mawakala kwa Bei nafuu lakini,sokoni Bei ikawa juu Hali ambayo itashindwa kutofautisha na maziwa ambayo yanatoka nje ya nchi na yanayozalishwa hapa nchini.

Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani Arusha alipotembelea kiwandani hapo kujionea uzalishaji wa maziwa,Mpina alisema kuwa serikali imeweka mazingira rafiki ya Biashara ili kuwezesha maziwa yanayozalishwa hapa nchini kufanya vizuri sokoni

"Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka huu kupitia wizara ya fedha tumeondoa tozo na Kodi mbalimbali ili kuwezesha Uwekezaji huu kuendelea kuleta tija na Matokeo chanya hapa nchini,hivyo tozo na Kodi sio tatizo tena Sasa jipanueni nchi zima hizi asilimia 70 hazitoshi fikisheni 100"alisema Mpina.

Aidha aliongeza kuwa Maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho ambayo hufahamika Kama Kilimanjaro  Fresh,yana Ubora ambao unatakiwa huku akiwataka kupelekea bidhaa hiyo katika mikoa ya dar es salaam,Mwanza na masoko yote ya ndani kwa kuwa uhitaji Ni mkubwa Sana.

Mpina alikipongeza kiwanda hicho kwa kununua maziwa kwa wafugaji kwa Bei inayoridhisha ya zaidi ya shilingi 800,kwani katika Bajeti ya wizara ya Mifugo na Uvuvi swala Bei liliwekwa kipaumbele.

Kwa Upande wake kaimu msajili wa bodi ya Maziwa Noely Byamungu,alisema kuwa uwepo wa kiwanda hicho ni muhimu katika kukuza uchumi wa wafugaji na Uchumi wa nchi.

Pia alisema kuwa kazi ya bodi hiyo ni kusimamia,kuratibu na kuendeleza tasnia ya Maziwa na wafugaji ikiwa Ni pamoja na kuhakikisha kuwa wafugaji wanafuga kisasa na kuzalisha malighafi zenye ubora unaohitajika sokoni.

Hasheem Said ambaye yupo katika kitengo cha Uendeshaji  kiwandani hapo  ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha viwanda na kufufua kwani  Vijana wamepata Ajira.

Hata hivyo ameiomba Serikali kusimamia Sera ya unywaji wa maziwa ili kuwezesha Watanzania kuongeza kiwango Cha utumiaji maziwa ili viwanda hivyo viweze kufanya vizuri zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post