TUME YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUJADILI UCHAGUZI MKUU

 

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Semistocles Kaijage akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kwenye  mkutano kati ya tume ya uchaguzi na vyombo vya habari ambapo amewataka kuzingatia maadili ya kazi zao, katika kutoa habari kipindi cha kampeni za uchaguzi ili kupunguza joto la kisiasa

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Semistocles Kaijage wa pili kutoka kulia akiwa na baadhi ya viongozi wa tume hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Tume hiyo Dkt. Wilson Mahela na kuroka kushoto ni Jaji mstaafu Thomas Mihayio na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi 

Mkurugenzi wa Tume hiyo Dkt. Wilson Mahela akizungumza na wahariri katika kikao hicho 

 Mkurugenzi wa Tume hiyo Dkt. Wilson Mahela akizungumza na wahariri katika kikao hicho  kutoka kushoto ni  Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na katikati ni Jaji mstaafu Thomas Mihayio kamishna wa tume hiyo. 

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakiwa katika picha kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bi. Giveness Aswile kulia akifuatilia mjadala katika kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.

Muongozaji wa kikao hicho Mroki Mroki akizungumza na kutoa utaratibu wa kikao hicho.

 

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Semistocles Kaijage amesema tume inatarajia kuona vyombo vya habari vikitoa kipaumbele kwa masuala yanayoelekea kujenga umoja wa kitaifa, badala ya habari ambazo zinaweza kuchochea vurugu kwani kalamu za wanahabari zisipotumika vizuri,zinaweza kuiingiza nchi kwenye machafuko kama ilivyotokea katika maeneo mengine. 

akizungumza katika mkutano uliokutanisha wahariri wa vyombo vya habari na tume ya uchaguzi ambapo amewataka kuzingatia maadili ya kazi zao, katika kutoa habari kipindi cha kampeni za uchaguzi ili kupunguza joto la kisiasa ambalo linaweza kuhatarisha amani na utulivu,

Jaji mstaafu Semistocles Kaijage ametoa Wito huo  leo Agosti 18, 2020  wakati wa kikao cha Tume hiyo na Wahariri wa vyombo vya habari kwa lengo la kutoa taarifa juu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu yalipofikiwa hadi sasa.

“Sheria za uchaguzi zipo, lakini sheria za nchi pia hazisimami kwa ajili ya uchaguzi,hakuna kitu kitakachoebda kinyume eti kwa sababu tu kuna uchaguzi, sheria za nchi zipo pale pale”, hivyo endapo kutajitokeza matendo ya jina yoyote yatachukuliwa hatua”, amesema Jaji Kaijage.

“Ninatarajia kuona vyombo vya habari hasa vya umma vinatenda haki sawa kwa vyama vyote kuhakikisha vinatoa nafasi kwa wagombea wote kujitangaza na kunadi sera na ilani za vyama vyao na kutoa Kipaumbele katika masuala yanayoelekea kujenga umoja wa kitaifa badala ya taarifa na habari ambazo zinachochea vurungu”, amesema Jaji Kaijage

Aidha, Tume imevitaka vyama vya siasa na wananchi kuheshimu sheria,katiba na taratibu za uchaguzi kwa kuhakikisha wanazifuata na kuzitelekeleza hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambapo sheria za nchi na uchaguzi zinaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Amesema, baadhi ya wananchi hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi watakuwa na joto kali la kisasa wanakuwa hawana utayari wa kuheshimu sheria na taratibu nawaza kufanya kampeni za kistaarabu zisizo ma vurugu na ni vema wote kutambua kuwa sheria za uchaguzi na nchi zinafuatwa.

Ameongeza kuwa, hadi sasa tume imekamilisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kifungu cha 15(5) cha sheria ya taifa ya uchaguzi ambao ulifanyika katika vituo 37,814 vya kuandikisha wapiga kura ambapo jumla ya wapiga kura wapya 7,326,552 waliandikishwa sawa na asilimia 31.63 ya wapiga kura 23,161,440 walioandikishwa Mwaka 2015.

Amesema, kufuatia idadi hiyo ya wapiga kura siku ya uchaguzi kutakuwa na vituo vya wapiga kura 80,155 na kila kituo kimoja kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500.

Pia amesema, Tume ya taifa ya uchaguzi imeandaa bajeti kiasi cha shilingi 331,728,258,035.00 ambazo zinatarajiwa kutumika katika uchaguzi Mkuu, fedha ambazo kwa asilimia mia moja zitagaramiwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mfumo Mkuu wa Hazina.

Naye , Mkurungezi wa Tume ya uchaguzi, Dk. Wilson Mahera amesema Tume hiyo inaendelea ma mchakato wa ununuzi wa vifaa na uchapishaji wa nyaraka mbalimbali za uchaguzi na kwamba hadi Sasa zabuni zimeishatagazwa na zinahusisha uchapishaji wa fomu mbalimbali za uchaguzi .

Pia amesema Tume hiyo imejipanga kukutana na wapiga kura ana kwa ana kwa kushiriki katika mikutano mbalimbali ili kuendelea kutoa elimu ya uchaguzi.

Post a Comment

Previous Post Next Post