AWESO ATAKA MIRADI YA MAJI ILIYOCHINI P4R KATIKA HALMASHAURI 86 IWE IMEKAMILIKA MWISHO WA SEPTEMBA 2020

 Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Nzega wakati wa ziara yake ya siku moja ya kufuatilia miradi ya maji iliyochini ya p4r. Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akisalimiana  na Katibu Tawala Wilaya ya Nzega Onesmo Kisoka wakati wa ziara yake ya siku moja ya kufuatilia miradi ya maji iliyochini ya p4r.

********************************

Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso amezitaka Halmashauri ya Wilaya 86 hapa nchini zilizopewa fedha za utekelezaji wa miradi ya kupeleka maji kwa wananchi zihakikishe miradi hiyo inakamilika kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.

Alitoa uamuzi huo  Nzega  na Igunga  mara baada kupata taarifa ya utekelezaji wa miradi ya P4r na kutoridhishwa na utekelezaji wake katika wilaya hizo ambao uko chini ya asilimia 40.

Aweso alisema Wizara ya Maji ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 119 toka Oktoba , 2019 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ya maji na hivyo wahandisi wa Mikoa na Halmashauri zilizopewa fedha hizo hawana sababu ya kujitetea juu ya uchelewashaji huo.

Naibu Waziri alisema kila Halmashauri ilipewa shilingi bilioni 1.3 ambapo zipo ambazo zimeshafika mbali na zipo ambazo ziko chini ikiwemo Nzega na Igunga.

Alisema Wahandisi wa Halmashauri ambazo muda utamalizika kabla ya miradi hiyo kukamilika watapaswa kutambua kuwa wamekosa sifa za kuendelea na nafasi zao kwa sababu ya kushindwa kutatua tatizo la kuwatua ndoo wakinamama kama Serikali ya awamu ya Tano ilivyokusudia.

Aweso aliongeza kuwa serikali ya Awamu ya Tano inahitaji matokeo na sio maneno katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.

Aliongeza kuwa Serikali iliingia Mkataba na Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kuhakikisha ifikapo Desemba mwaka huu, upatikanaji wa maji kwa maeneo ya vijijini uwe asilimia 85 na mjini asilimia 95 na hivyo lazima mkataba huo ukamilike kwa wakati.

Post a Comment

Previous Post Next Post