AWESO ASIMAMISHA BODI YA IGUWASA KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA

 NA TIGANYA VINCENT

Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso amesimamisha kazi kwa muda Mkurugenzi Mtendaji na Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Igunga(IGUWASA) kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa na watumishi dhidi yao.

Alitoa uamuzi huo juzi wilayani Igunga mara baada kukutana na watumishi wa IGUWASA ambao walitoa tuhuma mbalimbali ikwemo za rushwa ya ngono.

Baadhi ya tuhuma hizo ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu kuwatongoza watumishi wa kike wa Mamlaka na pindi wanapomkataa uwatishi kuwafukuza kazi.

Watumishi hao walitaja tuhuma nyingine ni kutumia fedha mbichi  za magati bila kuwasilisha benki na kumlazimisha Mhasibu atoe kiasi cha milioni 21 kwa matumizi binafsi na bila taratibu na baada ya kutaa kwa kushirikiana na Bodi akafukuzwa kazi. 

Kwa upande wa Bodi wamedai kuwa imekuwa ikishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji kuwanyanyasa watumishi ambao wanakuwa mstari kupinga vitendo viovu vya Mkurugenzi kwa kuwafukuza.

Walisema tuhuma nyingine za Bodi kutoa kwa ajira kwa  misingi ya upendeleo na wakati  bila kutangaza nafasi za ajira na kuwaacha walitumikia kwa mikataba kwa miaka zaidi ya mitano bila ajira.

Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kuunda Kamati ya kuchunguza tuhuma zilizotolewa na watumishi dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji na Bodi ili uongozi wa Wizara uweze kuchukua hatua.

Aweso alisema wakati Mkurugenzi Mtendaji huyo amesimamishwa nafasi yake itakaimiwa na Mhandisi Athumani Kilundumya wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Tabora (TUWASA)

Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akisalimiana  na Katibu Tawala Wilaya ya Nzega Onesmo Kisoka wakati wa ziara yake ya siku moja ya kufuatilia miradi ya maji iliyochini ya p4r.
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Nzega wakati wa ziara yake ya siku moja ya kufuatilia miradi ya maji iliyochini ya p4r.
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Igunga wakati wa ziara yake ya siku moja ya kufuatilia miradi ya maji iliyochini ya p4r.

Post a Comment

Previous Post Next Post