Mwandishi Wetu Kilimanjaro,
Waziri wa Afya, ππ‘π. ππ¨π‘ππ¦π¦ππ πππ‘ππ§π ππ«π°π (ππ), amewataka viongozi na wananchi kuimarisha elimu ya siasa na uraia kwa vijana na wanafunzi ili kuwajengea uzalendo, kuilinda nchi na kusimamia maslahi ya taifa. Amesema elimu hiyo ni muhimu katika kuandaa kizazi chenye uelewa na dhamira ya kulitumikia taifa kwa uadilifu.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro, akisisitiza kuwa kila mmoja ana jukumu la kulinda amani, umoja na rasilimali za nchi. Amesema viongozi waliokasimiwa mamlaka na Mheshimiwa Rais wanapaswa kusimamia kwa uaminifu maslahi ya taifa na kutokubali kushawishiwa na watu wenye maslahi binafsi.
Aidha, amewataka viongozi kuimarisha misingi ya chama na kufanya kazi kwa bidii ili kutatua changamoto za wananchi. Amesema changamoto za wananchi zinapopatiwa ufumbuzi, nguvu za watu wenye nia ya kuvuruga nchi hupungua, huku akisisitiza umuhimu wa viongozi kuzungumza kwa umoja katika matawi, kata na wilaya zao.
Waziri Mchengerwa amesema Tanzania inapaswa kuendelea kulinda na kutumia rasilimali zake kwa manufaa ya wananchi, akieleza kuwa hatua mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali zimeifanya nchi kuendelea kutumia rasilimali zake kwa maslahi ya taifa.
