Mwandishi Wetu,
Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo (Mb) ameonya vikali wanaohujumu mchakato wa mbolea za ruzuku huku akisisitiza serikali haitamvumilia yeyote anayechanganya mbolea bandia.
Akizungumza Makambako kwenye uzinduzi wa ghala la mbolea litakalohudumia mikoa ya kusini, amesema serikali itaendelea kuhakikisha wakulima wanapata mbolea bora kwa wakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent, amesema zaidi ya tani milioni moja za mbolea zimetumika nchini huku TFRA ikiendelea kushirikiana na wafanyabiashara wa pembejeo kuboresha upatikanaji wa mbolea kwa wakulima.







