
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Reuben Kwagilwa akiwasili kwa mara ya kwanza katika Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mji wa Serikali jijini Dodoma leo Aprili 09, 2026.
Mhe. Kwagilwa amepokelewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi, Naibu Makatibu Wakuu Bw. Abdallah Hassan Mitawi (Muungano), Balozi Baraka Luvanda (Mazingira), Menejimenti na Watumishi wa Ofisi hiyo.
Itakumbukwa kuwa Aprili 08, 2026 katila Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, Mhe. Kwagilwa aliapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo akichukua nafasi ya Mhe. Dkt. Festo Dugange aliyehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
