
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega (Mb) amewasili Mkoani Iringa kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Benjamin Sitta leo tarehe 25 Februari, 2026.
Katika ziara hiyo, Waziri Ulega atakagua Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na Miundombinu ya barabara na shughuli nyingine zinazotekelezwa katika Sekta ya Ujenzi.
