Aweso akabidhi tuzo za Umahiri kwa Mamlaka za Maji nchini

Mwandishi Wetu,

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amekabidhi tuzo kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira katika maeneo tofauti tofauti ya ufanisi na kupongeza  hatua kubwa ya maendeleo katika Sekta ya Maji.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imefanyika jijini Arusha ikishuhudiwa na wajumbe zaidi ya 1000 wanaoshiriki  Mkutano wa Wajumbe wa Bodi za Maji nchini, jijini Arusha.

Amesema watendaji bado wanajukumu la kuhakikisha wanavuka vikwazo vyote vilivyowakwamisha kufikia asilimia miamoja ya malengo waliyokusudia.

Amesema timu ya watendaji waliopo kwa sasa wanatia matumaini na nia ya dhati ya mapambano katika kuyafikia mafanikio inaonekana wazi.

Amesisitiza upendo kwa kila mmoja na kuongeza kuwa ndio msingi imara wa mafanikio.

Amesisitiza matumizi ya teknolojia na ubunifu katika kutatua changamoto za wananchi.

Tuzo za umahiri kwa Mamlaka za Maji za zimetolewa kwa kuzingatia maeneo tofauti tofauti ikiwemo uwezo wa kutatua changamoto za wananchi kwa haraka, uwezo katika kuwafikishia wananchi huduma ya majisafi na matumizi sahihi ya mapato.




Post a Comment

Previous Post Next Post