Naibu Katibu Mkuu Maji awataka Wajumbe Bodi za Mamlaka za Maji kuwa chachu ya mabadiliko

Mwandishi Wetu,

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Rose Ambrose Zacharia amewataka wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa Mamlaka za Majsafi na Usafi wa Mazingira nchini kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika maeneo yao.

Wito huo ametoa wakati akiwasilisha Salam za Wizara katika Mkutano wa Wajumbe wa Bodi hizo uliofanyika jijini Arusha.

Amesema jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha huduma za majisafi na salama zinawafikia watanzania wote zinaonekana wazi hivyo wajumbe wanapaswa kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa kujituma.

Amesema Wizara Ina Imani kubwa na wajumbe hao hivyo majadiliano ndani mkutano huo yalenge kupiga hatua mbele katika kuyafikia malengo.

Mkutano wa Wajumbe wa Bodi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini unatarajiwa kufunguliwa kesho Feb. 24, 2026. Mgeni Rasmi ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb)


Post a Comment

Previous Post Next Post