
TANAPA ni taasisi muhimu sana katika uhifadhi wa maliasili nchini Tanzania, na hili nitaendelea kulisema kila mara katika mijadara mbalimbali vile vile tumeendelea kufanya nalo kazi kwa ukaribu ili kulinda mazingira, wanyamapori na tunu zote zilizomo ndani ya Hifadhi za Taifa kwa manufaa ya Tanzania na dunia kwa ujumla.”
Kauli hiyo imedadavuliwa na Mr. Shigeki Komatsubara Mwakilishi Mkazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) alipotembelea banda la TANAPA wanaoshiriki Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar ( ZITF) katika viwanja vya Dimani – Fumba. Maonesho yaliyoanza desemba 29, 2025 na yanatarajiwa kuhitimishwa Januari 16, 2026.
Aidha, banda hilo pia limetembelewa na viongozi mbalimbali kupata elimu ya uhifadhi na uwekezaji, pamoja na kuhamasishwa kutembelea vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya Hifadhi za Taifa, miongoni mwao ni Mhe. Hamida M. Khamis, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja na Masoud M. Faki Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Zanzibar.
