MHANDISI MASAUNI ASISITIZA MANUFAA YA MUUNGANO

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza wakati akifungua Semina kuhusu Muungano kwa wahariri wa vyombo vya habari Zanzibar, Disemba 19,2025.


Baadhi ya wahariri na viongozi walioshiriki Semina kuhusu Muungano kwa wahariri wa vyombo vya Habari Zanzibar iliyofanyika Disemba 19, 2025

Na. Mwandishi Wetu,Unguja

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Serikali itaendelea kuimarisha Muungano ili kuleta manufaa kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya waasisi.

Amesema tangu kuasisiwa kwake Muungano umeendelea kuimarisha Umoja na mshikamano na kuleta mafanikio makubwa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii na hivyo kukuza uhusiano baina ya Tanzania na Jumuiya za Kimataifa.

Mhe. Masauni amesema hayo Desemba 19, 2025, wakati akifungua Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari wa Zanzibar na kusisitiza miaka 61 ya Muungano imeleta faida kubwa katika kuimarisha maisha ya wananchi na jamii kwa ujumla.

Amesema Vyombo vya Habari vina wajibu wa kuhakikisha taarifa zinazoandikwa kutangazwa kuhusu Muungano zinajikita katika kujenga umoja wa kitaifa sambamba na kuitisha mijadala yenye taswira chanya katika kuwaweka pamoja Watanzania.

Semina hii itakuwa na matokeo chanya katika kukuza uelewa kuhusu Muungano na kuendelea kuuenzi na kuudumisha kwa kuzingatia Sekta ya Habari ina wajibu wa vyombo vya habari ambao ni kuhabarisha na kuelimisha” amesema Mhe. Masauni.

Aidha amesema vyombo vya habari vina wajibu pia wa kuzingatia maadili, sheria na taratibu zilizowekwa kwa kuzingatia Katiba hususani Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayohusu haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari.

Ameeleza kuwa vyombo vya habari vna wajibu wa kuenzi misingi ya Muungano iliyowekwa na Waasisi wake, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ili kuendelea kuwa nguzo ya kuimarisha umoja, amani na mshikamano ili kujenga uchumi imara.

Kwa upande wake mwanasiasa mkongwe nchin, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema sababu ya uwepo wa Muungano ni pamoja na umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na hivyo kuwawezesha Watanzania kuendelea kuishi kwa umoja, upendo na mshikamano.

PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

 

Post a Comment

Previous Post Next Post