DKT. KIJAJI AWASILI IRINGA KWA ZIARA YA KIKAZI

 

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), leo 18 Disemba, 2025 amewasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa tayari kuanza ziara ya kikazi katika mkoa huo

Waziri Dkt. Kijaji ameambatana na Naibu wake Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nkoba Mabula, viongozi mbalimbali wa Wizara sambamba na Viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)

Ujumbe wa ziara hiyo utatembelea miradi mbalimbali ya uhifadhi iliyopo kwenye Hifadhi ya Taifa Ruaha 

Aidha, Dkt. Kijaji ameahidi kushirikiana na mkoa wa Iringa kuendeleza uhifadhi na kutangaza vivutio vya utalii vilivyomo kwenye mkoa huo ili kuongeza chachu katika ukuaji wa uchumi wa mkoa na Taifa kwa jumla ili wananchi waendelee kunufaika na rasilimali zao.    

Post a Comment

Previous Post Next Post