Mwandishi Wetu,
Jumla ya wananchi 20 kutoka Mkoa wa Dar es salaam na Pwani wamenufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Kanda ya Mashariki, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mwakilishi wa Ruzuku wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, Bi.Claudia Morand alisema miongoni mwa wananchi walionufaika, wananchi 5 walisajiliwa kwenye daftari la wakulima, wafanyabiashara 10 walielekezwa namna ya kuhuisha leseni zao za biashara katika mfumo na wananchi 3 walipata mafunzo ya kuanzisha biashara ya mbolea (kuingiza nchini na kusambaza)
Zoezi hilo lilifanyika kwa siku 2 tarehe 18 na 19 Juni 2025 katika Soko la Kisutu, jijini Dar es Salaam.