Mwandishi Wetu,
Jumla ya wananchi 20 kutoka Mkoa wa Dar es salaam na Pwani wamenufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Kanda ya Mashariki, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wap Umma.
Zoezi hilo lilifanyika kwa siku 2 tarehe 18 na 19 Juni 2025 katika Soko la Kisutu, jijini Dar es Salaam.