NA MWANDISHI WETU
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa tuzo za 32 za utalii wa kimataifa ukanda wa Afrika na Bara la Hindi ambapo tukio hilo litafanyika katika hoteli ya Johari rotana jijini Dar es salaam juni 28 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mkurugenzi wa (TTB) Emphraim Mafuru amesema kuwa Tanzania imepewa heshima kubwa ya kusimamia tuzo za utalii ambapo kampuni mbalimbali zitashiriki kwenye kunia tuzo hizo ikiwemo
"Tanzania imekuwa nchi pekee katika ukanda wa Afrika katika kuwania tuzo za utalii ambapo ni kitovu cha utalii katika bara la Afrika na ndio nchi pekee iliyoshinda tuzo nyingi sambamba na kuwa mwenyeji wa tuzo hizi nchi zingine zitakazo shiriki ni pamoja na Mexico, Italia , Hong Kong na Umoja wa Falme za kiarabu," amesema Mafuru
Aidha mkurugenzi huyo ameeleza kuwa tuzo hizo zilianzishwa mwaka 1993 ambapo lengo lake ni kutambua mchango wa wadau katika sekta ya utalii ambapo Duniani sekta ya utalii umetajwa kuwa na mazao mbalimbali ikiwemo utalii wa wanyama pori , utalii wa michezo na utalii wa mikutano.
Hata hivyo Tanzania imepata fursa ya kuonyesha mazao mbalimbali kama vile utalii wa tiba ,utalii wa usafiri wa ardhi na usafiri wa anga ambapo tuzo hizo zitafanyika kwa levo ya Kanda.
Aliendelea kuwa mwaka Jana shughuli tuzo kama hizi zilifanyika Mombasa nchini Kenya ambapo Tanzania ilijishindia tuzo tano ikiwemo Bodi Bora Afrika ilikuwa bodi ya utalii Tanzania (TTB), kivutio bora cha utalii Afrika ulikuwa mlima Kilimanjaro na hifadhi Bora Afrika ilikuwa mbuga ya wanyama ya Serengeti.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Hospitali ya Shifaa, Victoria Tarimo amesema kuwa wao kama watabibu wako tayari kupokea ugeni pamoja na kutoa huduma ya kwanza kimataifa.
Amesema kuwa hospitali yao ina huduma safi pamoja na uweledi wa utoaji huduma kwa viwango vya hali ya juu ambapo ina vifaa vya kisasa, kama vile machine bora sambamba na wataalamu wabobezi kwenye sekta ya afya.
Naye Meneja Mkuu wa Hoteli ya Johari Rotana Ahmed Said, amesema kuwa wanajivua kuwa na hoteli kubwa yenye viwango vya hali ya juu katika kuwahudumia wateja wao
Hivyo ameendelea kueleza kuwa wataendelea kuboresha huduma zao kipindi chote cha tuzo hizo Ili kuwa na viwango Bora na vya kisasa na kuweza kuvutia wateja wa ndani na nje ya Tanzania



