JAMII YAASWA KUFICHUA WAFANYABIASHARA ZA MAGENDO BAGAMOYO

 Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imepewa rai ya kuzungumza na wenyeji wa Bagamoyo ili kuwaelimisha juu ya athari za kukwepa kodi na magendo.

Rai hiyo imetolewa Machi 3, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga alipokuwa akizungumza na Maofisa wa Mamlaka hiyo walipokuwa wakitoa elimu ya mlipa kodi kwa wakazi wa Bagamoyo.

DC Ndemanga amesema kuwa mapato ya serikali zaidi yanayopotea kutokana na watu kukwepa kodi kwa kupitisha mizigo kwa njia ya magendo kwenye bandari ya Bagamoyo ni mengi sana, kama watu wengi wanhekuwa wanapita pale bandarini Bagamoyo TRA ingekuwa inakusanya Bilioni tatu hadi nne kwa mwezi.

"Unaona jahazi limetia nanga pahala ambapo sio bandari badala ya kutoa taarifa nao wanakwenda kusaidia kushusha bidhaa ili wapate chochote hawa wananchi nao wanaihujumu serikali", amesema Ndemanga.

Ndemanga amesema kuwa Mamlaka itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya hatari ya kupitisha mizigo yao kwa njia za magendo

"Hawa wafanyabiashara wakielewa hawatakubali mizigo yao ipitishwe njia za magendo kwa sababu tukikamata hasara itamkumba yeye na sio wale wanaowatuma" amesema.

"Wengine wanatumia namba ya mlipa kodi ya mtu mwengine sisi tunahesabu mtu huyo naye anafanya magendo tu", ameongza Ndemanga

Naye Deogratius Nyenshile Ofisa wa Forodha wa TRA ambaye ndiye aliyeendesha mafunzo hayo amesema kuwa upo umuhimu kwa jamii kujua athari za kiuchumi endapo watu wanakwepa kodi .

"Mwananchi ndio mlinzi wa kwanza "wasipoelimishwa wanaweza kushiriki kwenye biashara ya magendo bila yeye mwenyewe kujua kwa hiyo ni muhimu kila wakati kuwaelemisha wanachi madhala ya ukwepaji kodi na magendo kwenye ustawi wa Taifa nchini " amesema Nyenshile.

Amesema kuwa mamlaka itaendelea na jitahada hizo za kutoa elimu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa mstari wa mbele kwenye kufichua magendo.

Naye Mwenyekiti wa Wabeba mizigo katika bandari ya Bagamoyo Jumanne Buna ametoa malalamiko yake kuwa wafanyabiashara wadogo wanashindwa kuendelea na bishara zao kwa kutozwa kodi sawa na wafanyabiashara wakubwa .






Post a Comment

Previous Post Next Post