Tanzania Yazindua Bodi ya Wakurugenzi ya Nguvu za Atomiki kwa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akizungumza wakati wa uzinduzi akitoa cheti kwa Mwenyekiti wa bodi ya Tume za Atomiki Tanzania (TAEC) Joseph Msambichaka leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi ya tume hiyo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi ya tume za Atomiki, uzinduzi ulioifanyika jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Najat Kassim Mohammed akizungumza akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi ya tume za Atomiki, uzinduzi ulioifanyika jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 2024.
Mwenyekiti wa bodi ya Tume za Atomiki Tanzania (TAEC) Joseph Msambichaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi ya tume za Atomiki, uzinduzi ulioifanyika jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 2024.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi chati Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu

TUME ya Nguvu za Atomiki imezindua rasmi Bodi ya Wakurugenzi ya Nguvu za Atomiki, ikiwa ni hatua muhimu inayolenga kusimamia na kuendeleza matumizi salama na yenye tija ya teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo ya taifa.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 2025 ukihudhuriwa na viongozi wa serikali, wataalamu wa sayansi na teknolojia na wadau wa sekta ya nishati, wadau wa elimu na afya.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa umuhimu wa bodi hiyo katika kuhakikisha matumizi salama na endelevu ya teknolojia ya atomiki kwa maendeleo ya sekta mbalimbali kama afya, kilimo, viwanda, na nishati.

"Uzinduzi wa bodi hii ni hatua muhimu kwa Tanzania katika kuhakikisha kuwa tunaendelea kunufaika na teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya amani. Pia uangalie mahusiano ya vyuo vikuu na tume katika kushirikiana na kuongeza jitihada katika tafiti mbalimbali. Tunaangazia matumizi katika afya kwa uchunguzi wa maradhi kama saratani, katika kilimo kwa kuboresha mbegu, na hata viwandani kwa mchakato wa uzalishaji wa bidhaa." Amesema Prof. Mkenda.

Pia ametoa wito kwa taasisi za urekebu, wasimamizi wa kanuni, taratibu na kukagua kusimamia sera, miongozo, na usimamizi wa matumizi ya mionzi na teknolojia ya nyuklia nchini, huku ikizingatia usalama wa mazingira na wananchi.

Bodi hiyo inatarajiwa kushirikiana kwa karibu na taasisi za elimu ya juu na vyuo vya utafiti ili kuhakikisha kuwa wataalamu wa Kitanzania wanapewa mafunzo na ujuzi wa kisasa kuhusu teknolojia ya atomiki.

Pia amewaasa wasijewakachanganya nyezo na lengo la tozo katika maeneo mbalimbali ambapo wanatakiwa wasafirishaji wa bidhaa mbalimbali kutolewa tozo.

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Joseph Msambichaka ambaye ni mtaalamu wa masuala ya nishati na mionzi, aliwahakikishia Watanzania kuwa bodi hiyo itafanya kazi kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na miongozo ya Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).

"Tanzania imepiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo. Bodi yetu itahakikisha kuwa tunafuata viwango vya kimataifa vya usalama na ubora katika sekta hii nyeti," amesema Mwenyekiti wa bodi.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Najat Kassim Mohammed Serikali imedhamiria kuimarisha matumizi ya teknolojia ya atomiki kwa maendeleo ya taifa kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa na wadau wa sekta mbalimbali.

Pia amesema kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha kwa wajumbe wa bodi waliokaguliwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post