Mwandishi Wetu,
Wakulima wa pamba wilayani Chato, Geita wamefurahishwa na mpango wa ruzuku ya mbolea unaotekelezwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).
Wamesema mpango huo umeongeza uzalishaji wa pamba na kuboresha maisha yao!
Katika ziara ya Bodi ya TFRA tarehe 18 Februari 2025, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Anthony Diallo, wakulima wa vijiji vya Necezi na Songambele walieleza namna mbolea ilivyobadili maisha yao kupitia kilimo cha pamba.
✅ Mavuno yameongezeka – Sasa wakulima wanavuna hadi kilo 2000 kwa ekari moja kutoka mavuno ya kilo 200
✅ Elimu ya matumizi sahihi ya mbolea inatolewa ambapo Maafisa ugani wamewasaidia wakulima kutumia mbolea ipasavyo.
✅ Upatikanaji wa mbolea umeboreshwa baada ya TFRA imeweka bei elekezi kwa kuzingatia umbali wa kijiji kutoka makao makuu ya Wilaya na inashirikiana na wadau kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima kwa wakati.
Mkulima Saimoni Lutabeka wa Kijiji cha Songambele amesema:
"Nilianza kutumia mbolea aina ya NPK kutoka Minjingu, sasa navuna zaidi na maisha yangu yamebadilika na kumpelekea kupata tuzo ya trekta kwa kutambulika kama mkulima wa mfano wa zao la pamba!"
TFRA inaendelea kusimamia mpango huu kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) ili kuhakikisha wakulima wanapata elimu sahihi na pembejeo bora kwa wakati.
Serikali imejipanga kuendelea kuwawezesha wakulima! Je, wewe ni mkulima wa pamba? Tuambie uzoefu wako naruzuku ya mbolea! 👇🏽🌾