TANAPA YASHIRIKI MAONESHO YA ZANZIBAR TOURISM SUMMIT

 

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeshiriki maonesho ya 3 ya Zanzibar Tourism Summit & B2B Expro (ZTS) yaliyozinduliwa na Mheshimiwa Mudrick Ramadhani Soraga, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar tarehe 18/02/2025 katika kisiwa cha Unguja. Maonesho haya yamehitimishwa tarehe 20/02/2025.

Aidha, maonesho hayo yamekutanisha kampuni za kitalii takribani 100 kutoka zaidi ya nchi 21 pamoja na wadau mbalimbali wa utalii. TANAPA ilitumia maonesho hayo kunadi vivutio vya utalii vinavyopatikana katika Hifadhi za Taifa, elimu ya uhifadhi pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana ndani ya Hifadhi za Taifa.

Maonesho ya Zanzibar Tourism Summit & B2B Expro ni jukwaa kubwa linalowakutanisha wadau wa utalii kutoka mataifa mbalimbali kwa lengo la kutangaza vivutio, kuimarisha ushirikiano, na kufanikisha biashara katika sekta ya utalii. Ushiriki wa TANAPA katika maonesho hayo umefungua wigo mpana katika utoaji wa taarifa kwa wadau na wageni mbalimbali walioshiriki maonesho hayo.   

Post a Comment

Previous Post Next Post