SERIKALI: TAASISI 551 ZATUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

 

 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali wakati wa Kikao cha 12 cha Mkutano wa 18 wa Bunge jijini Dodoma leo Februari 12, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati Kikao cha 12 cha Mkutano wa 18 wa Bunge jijini Dodoma leo Februari 12, 2025.

……….

Jumla ya taasisi 551 zimeanza matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ikiwa ni katika jitihada za kuunga mkono Serikali kupunguza ukataji miti na kulinda afya za wananchi.

Hatua hiyo, ni katika utekelezaji wa katazo la matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi za Umma na Binafsi zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi ya mia moja

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Februari 12, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Rungwe Mhe. Anton Mwantona aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha taasisi zinazohudumia watu wengi zinaweka mifumo ya majiko ya gesi ili kuokoa mazingira.

Akiendelea kujibu swali hilo, Naibu Waziri Khamis amesema Serikali tayari imesaini makubaliano ya awali na wawekezaji mbalimbali ikiwemo makampuni ya Oryx, Taifa Gas, Lake Gas na Manji’s gas kuhusu kutoa ruzuku ya shilingi bilioni 8.64 kwenye nishati safi ya kupikia.

Mhe. Khamis amefafanua kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza mzigo wa gharama kwa watumiaji wa nishati safi ambapo jumla ya majiko 452,455 yamepata ruzuku.

Aidha, amesema Serikali inaendelea na ukamilishaji wa taratibu za kuanzisha Mfuko wa Nishati safi ya kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu bei ya gesi. 

Hivyo, Mhe. Khamis amesema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha uandaaji wa Kanuni ya Katazo la Matumizi ya Kuni na Mkaa kwa Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kwa siku zitakazojumuisha taasisi za umma na binafsi. 

Akijibu swali la nyongeza la Mhe. Mwantona aliyetaka kufahamu kama Serikali iko tayari kutoa ruzuku kwa wawekezaji wakubwa ili taasisi zenye watu zaidi ya 100 zikawekewa majiko ya gesi, Naibu Waziri Khamis amesema Serikali imeweka mpango madhubuti wa kutekeleza mkakati wa kuhakikisha jamii inahamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema kuwa ili kufanikisha hatua hiyo, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia (Cook Fund) utakaowezesha taasisi, vikundi na watu binafsi kuwezeshwa ili kupata majiko pamoja na kuwekewa miundombinu ya nishati safi ya kupikia.

Pamoja na hatua hiyo ameongeza kuwa tayari Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa miaka 10 (2024-2034) ambao unatoa mwongozo wa utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia umezinduliwa.

Tayari mkakati wa miaka 10 kusaidia kutumia niushati safi 

Post a Comment

Previous Post Next Post