e-GA YATOA TUZO KWA TAASISI VINARA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

 


MAMLAKA ya Serikali Mtandao yatoa Tuzo kwa Taasisi Vinara kwenye utekelezaji wa Serikali Mtandao mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imetoa tuzo kwa Taasisi za Umma zilizofanya vizuri katika utekelezaji wa Serikali Mtandao ikiwa ni sehemu ya mipango ya Serikali ya kuchochea matumizi TEHAMA Serikalini ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa Tuzo hizo katika Kikao kazi cha 5 cha Serikali Mtandao kilichofanyika jijini Arusha, Meneja wa Usimamizi wa Udhibiti na Viwango vya Serikali Mtandao Bi. Sultana Seiff amesema Mamlaka iliweka vigezo mbalimbali ambavyo vilizingatiwa katika upatikanaji wa Taasisi zilizofanya vizuri katika Utekelezaji wa Serikali Mtandao.

Amesema Tuzo hizo ziligawanyika maeneo makuu matatu (3) ya utekelezaji wa Serikali Mtandao ambayo ni Uzingatiwaji wa Sheria ya Serikali Mtandao, Viwango na Miongozo yaani “Best Performance in Compliance to e-Government Act, Standards and Guidelines” Taasisi Hodari kwenye Matumizi ya TEHAMA katika kuwashirikisha Wananchi- “Best Performance in Utilization of ICT for Citizen Engagement” na Taasisi Kinara katika Kuunganisha na kubadilishana Taarifa kupitia Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini ujulikanao kama GoVESB “Best Performance in e-Government System Integration through GovESB”

Bi. Seiff amesema katika kundi la kwanza, waliangalia maeneo mawili ambayo ni Taasisi zilizopo katika ngazi ya NNE ya Ukomavu wa TEHAMA Serikalini yani Level 4 of e-Government Capability Maturity na Taasisi zilizopo katika ngazi ya TATU ya Ukomavu wa tehama Serikalini yaani Level 3 of e-Government Capability Maturity Framework.

Katika ngazi ya nne ya Ukomavu wa tehama washindi wa nne waliibuka ambao ni Wizara ya Katiba na Sheria akishika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) mshindi wa pili, Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) mshindi wa tatu na Mamlaka ya Bandari (TPA) mshindi wa nne.

Aidha, kwa upande wa Taasisi zilizo katika ngazi ya tatu Geita District Council aliibuka mshindi pekeee katika ukomavu wa matumizi ya tehama.

Bi. Seiff alisema kwa upande wa Taasisi Hodari kwenye Matumizi ya tehama katika kuwashirikisha wananchi kupata huduma bora za Serikali yaani Best Performance in Utilization of ICT for Citizen Engagement; Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) aliibuka kinara nafasi ya kwanza, huku Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) akishika nafasi ya pili na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuchukua tuzo nafasi ya tatu.

Na taasisi ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (National Council for Technical and Vocational Education and Training) (NACTVET) aliibuka mshindi pekee kwa Taasisi zilizofanya vizuri katika Kuunganisha na Kubadilishana Taarifa kupitia Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini ujulikanao kama GoVESB yaani Best Performance in e-Government System Integration through GovESB.



Post a Comment

Previous Post Next Post