
………..…..
Na Sixmund Begashe – Ngorongoro
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Cuba inaendeleza jitihada za kuimarisha Uhifadhi katika eneo la Ngorongoro Mkoani Arusha kwa kutafuta utatuzi wa kudumu wa Mimea Vamizi.
Katika kuhakikisha changamoto hiyo inapatiwa ufumbuzi wa kudumu, juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, zimewakutanisha watafiti kutoka nchini Cuba na wa Wizara hiyo katika Bonde la Kreta lililopo ndani ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro ili kujionea ukubwa wa changamoto hiyo.
Akizungumza na wataalam hao kutoka Cuba kwa niaba ya wataam wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Emmanuel Msofe licha ya kuwapongeza kwa moyo wao wa kuungana na wataalam wa Wizara hiyo katika zoezi hilo, amewahakikishia kuwa Wizara ipotayari kupokea ushauri wao wa kutatua changamoto ya Mimea Vamizi hivyo wasisite kufanya hivyo.
Aidha, akizungumza baada ya kujuone hali halisi katika bonde hilo, Kiongozi wa timu ya wataalam kutoka nchini Cuba, Dkt. Orlando Enrique Sanchez Leon ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwashirikisha katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo, na kuwathibitishia kuwa wao kama wataam watashirikiana bega kwa bega katika kuhakikisha changamoto hiyo inakwisha.
Naye Kaimu Meneja Kitengo cha Usimamizi wa Wanyamapori na Utafiti, Afisa Uhifadhi Mkuu, Lohi Zakaria alieleza kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kudhibiti mimea hiyo vamizi katika Bonde hilo pekee Duniani hata hivyo jitihada hizo hazikufanikiwa hivyo ujio wa Wataalam hao ni faraja kubwa kwa Uhifadhi endelevu, hali itakayo imarisha Utalii.
Wakiwa ndani ya Bonde hilo, wataalam hao walijionea namna mimea vamizi ijulikanayo kwa majina ya kitaalam ni pamoja na Bidens Schimperri
Gutenbergia Cordifolia
Datura Stramonium
Tagetis Minuta (Bangi pori)
Verbena officinalis, ikiwa imeota sehemu mbalimbali hali inayopelekea Wanyamapori kushindwa kupata malisho kwenye maeneo hao.