Wafanyabiashara wa mbolea watakiwa kuzingatia bei elekezi

Mwandishi Wetu,

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent, anapenda kuwafahamisha wadau wote wa tasnia ya mbolea nchini – waingizaji, wazalishaji, wafanyabiashara wa mbolea, na wakulima – kuwa bei elekezi za kuuzia mbolea ni zile zilizotangazwa na Mamlaka tarehe 15 Novemba 2024.

Bei hizi elekezi zinapatikana kupitia:

👉 Tovuti ya Wizara ya Kilimo: www.kilimo.go.tz

👉 Tovuti ya TFRA: www.tfra.go.tz

Wafanyabiashara wote mnakumbushwa kuuza mbolea kwa bei elekezi iliyotolewa au chini yake.

Imetolewa na:

MAMLAKA YA UDHIBITI WA MBOLEA TANZANIA (TFRA).





Post a Comment

Previous Post Next Post