Ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale anayejulikana kama Zinjanthropus boisel Katika bonde la Olduvai Hifadhi ya Ngorongoro ndio ullofungua milango ya tafiti nyingi za mambo kale na kubadilisha uelewa wa wanasayansi kuhusu mchango wa Tazania na bara la Afrika katika historia na chimbuko la binadamu duniani.
Katika picha Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro bwana Abdul-Razaq Badru (Kushoto) na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania profesa Hamisi Masania Malebo (Kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Duke nchini Marekani Profesa Charles Musiba kuhusu mchango wa Zinjathropus katika utafiti duniani.
Fuvu la Zinjanthropus lenye umri wa miaka milioni 1.75 lililogunduliwa mwaka 1959 na Dr. Mary Leakey na hili ndio fuvu la kwanza la jamii ya "Paranthropus" hivyo wakampa jina la kiasili Fuvu la Zinjanthropus lenye umri wa miaka milioni 1.75 lililogunduliwa mwaka 1959 na Dr. Mary Leakey na hili ndio fuvu la kwanza la jamii ya "Paranthropus hivyo wakampa jina la kiasili (nick-name) Zinj, ikimaanisha mtu wa Afrika.
Ugunduzi huu ulitangazwa katika majarida mbalimbali ya kimataifa na kuandikwa kwenye vitabu vya kufundishia katika shule za msingi na sekondari ndani ya nchi na hata mataifa ya nje, hivyo kuchochea tafiti za malikale na kuendeleza utalii wa nchi na dunia kwa ujumla.
Kutokana na upekee na umuhimu wa Fuvu la Zinjanthropus mwaka 1970 wakati wa maonesho ya EXPO Japan fuvu hili lilipata nishani ya dhahabu
Fuvu hili limeendelea kuvutia wasomi mbalimbali na wataalam kutoka ndani na nje ya nchi kufanya utafiti wa masailia ya malikale katika bonde la Olduvai ambalo kwa sehemu kubwa bonde hill limechangia wasomi wengi kupata shahada za Uzamivu (PhD) kutokana na tafiti zao.

