Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) zimepokea kwa mara ya pili cheti cha ubora cha kukidhi viwango vya Ithibati ya kimataifa ya utendaji kazi cha ISO 9001,2015.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vyeti hivyo iliyofanyika katika makao makuu ya shirika la hifadhi Taifa Tanzania Tanapa, Mkuu wa kitengo cha utalii Tanapa Jully Lyimo amesema kuwa hifadhi za kanda ya Kaskazini ndizo zimeongoza kukidhi viwango hivyo.
Ametaja hifadhi hizo kuwa ni makao makuu ya shirika la hifadhi za Taifa Tanzania kanda ya kaskazini,hifadhi ya Arusha,Mkomazi,Tarangire ,Ziwa Manyara na Kilimanajro ambapo kiwango hicho cha kimataifa kinaangalia huduma mbali mbali zinazotolewa na hifadhi hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la viwango Tanzania,Dokta Ashura Katunzi amesema kuwa shirika hilo limepokea vyeti saba ambapo vingine ni miongoni mwa vituo 21 walivyo navy huku akisisitiza mashirika mengine kuwa na weledi katika utoaji wa huduma.
Aidha ametoa.rai kwa shirika hilo kuhakikidja ithibati hiyo inaleta manufaa makubwa ikiwemo kuongeza ujasiri kwa wateja na watalii wanaowahudumia na wale wanaopata huduma za shirika hilo.
Aidha dkt Ashura amesema kuwa utoaji wa cheti hicho umekuwa hauzingatii ukubwa au udogo wa shirika hivyo ni vyema taasisi nyingine za umma zithibitishe mifumo uao ili kujiweka katika viwango bora vya utoaji huduma .
Naye Naibu kamishna wa uhifadhi Tanapa Massana Mwishawa amesema kuwa lengo la Tanapa ni kuhakikisha hifadhi zote 21 za Tanapa zinakaguliwa na zinapata vyeti vya Ithibati ya kimataifa na wamejipanga ndani ya miaka mitatu watatangaza kuwa hifadhi hizo zimepata kiwango .
Amessma kuwa katika kipindi cha miaka 3 idadi ya watalii na mapato yanaongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya watalii walikuwa 997,873 na mapato yalifikia shs 174,715,158,493.75 mwaka 2022/2023 ambapo jumla.ya watalii walikuwa 1,670,437 na mapato yalikuwa shs 337,434,076,896.29.
Hata hivyo.miongoni mwa vituo vilivyopokea vyeti hivyo ni pamoja na hifadhi ya Mkomazi ambapo Emmanuel Mwinara Kamishna msaidizi wa uhifadhi na Mkuu wa hifadhi hiyo amesema kuoewa cheti hicho kwa awamu ya pili inamsaidia kuwa na imani katika utoaji wa huduma bora.