NISHATI SAFI YA KUPIKIA YA RAFIKI BRIQUETTES YAACHA ALAMA TEMEKE


Shirika la Madini la Taifa STAMICO lafamya kampeni ya kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini ili kuokoa mazingira na balaa la ukataji miti.

Akiongea kuhusu kampeni hiyo iliyofanyika Desemba 22, kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Wilayani Temeke Mstahiki Meyaa wa Manispaa ya Temeke Ndugu Abdalla Mtinika ameipongeza STAMICO kwa kushiriki moja kwa moja kuzalisha Nishati safi na kuhamasisha matumizi yake ili kuleta mabadiliko kwa watanzania.

Amesema STAMICO imepiga hatua mbele katika kufuata maelekezo ya Serikali ya kwamba ifikapo Disemba 31, 2024 Taasisi zinahudumia watu zaidi ya 100 ziache kutumia nishati chafu na kugeukia nishati safi.

Amesema kwa kuleta Nishati hii STAMICO imefanya Mapinduzi yatakayoacha alama kwa kizazi kijacho kwa kuwa mazingira yatabaki kuwa salama kwa maisha ya watu

Ametoa shime kwa Serikali kuendelea kuwekeza kwenye mitambo ya uzalishaji ili kuipa Nguvu STAMICO na kuiwezesha kuwa na kiwanda katika kila mkoa kwani hii itasaidia kuokoa idadi kubwa ya miti ambayo inateketea kwa kutengeneza nishati ya kupikia

Akiongea kuhusu Rafiki Briquettes Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema Chimbuko la kampeni hii ya kuhamasisha ni kuunga mkono maono ya Serikali ya kupunguza matumizi ya nishati zitokanazo na Miti na kugeukia nishati safi.

" Tumeona kuna haja ya kila mtanzania kushiriki kati suala la matumizi ya nishati Ndio maana tukaja na kauli mbiu ya Zima Kuni na Mkaa Washa Rafiki Briquettes" Alisema Dkt.Mwasse

Ametumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote wa STAMICO wakiwemo mawakala na wanunuzi wa Rafiki Briquettes kwa kushirikiana bega kwa bega na Shirika hilo.

Ameongeza kuwa kampeni hizi zimeenda sambamba utambuzi wa mawakala na utoaji Veti kwa mawakala ili kuhakikisha mkaa huu umawafikia wengi

Aidha, Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Dar es Salaam

Mhe. Janeth Masaburi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuichukua ajenda hii ya dunia ya kulinda mazingira kwa kutumia nishati safi na salama.

Kwa upande wa watumiaji wa nishati hii Sajenti Yohana Semwenda amesema mkaa huu una manufaa kwa kuwa unadumu zaidi na umekuja kuondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa nishati ya kupikia.

"Rafiki Briquettes hii ni Rafiki kweli kweli kimatumizi kwa kuwa tangu tumeanza kutumia tumeona mkaa huu ni rafiki na salama kwani hauna moshi, unatumia mkaa mchache kupika chakula kingi na unawaka kwa muda mrefu."

Amesema Semwenda

STAMICO imeenda kufanya kampeni hii Temeke ili wanatemeke waweze kuchangamkia fursa zinazotokana na nishati hiyo kushiki katika ajenda ya Kutunza mazingira.

Post a Comment

Previous Post Next Post