Kamishna Mkuu wa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Yusuph Mwenda, akimkabidhi Makaunta kwaajili ya shule Mkurugenzi wa Kituo cha New Faraja, Zamda Idrisa Juma pamoja na mtoto wa kituo cha New Faraja leo Desemba 21, 2024 TRA walipofika kutoa zawadi ya Kristmasi na Mwakampya.
Kamishna Mkuu wa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Yusuph Mwenda akimkabidhi moja vitu mbalimbali walivyofika navyo walipotembelea kituo cha Mother Teresa kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam leo Desemba 21, 2024.
Vyakula na Vitu mbalimbali vilivyotolewa na TRA.
Kamishna Mkuu wa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Yusuph Mwenda akizungumza na watoto waliopo katika kituo cha kulele watoto Yatima na wanaoishi Mazingira hatarishi cha New Faraja kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam leo Desemba 21, 2024.
KATIKA kurudisha kwa Jamii Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Desemba 21, 2024 imetoa zawadi ya Krismasi na Mwaka mpya kwa Vituo viwili vya watu wenye mahitaji Maalumu na watoto Yatima na Wanaoishi Mazingira Hatarishi ambavyo ni kituo cha Mother Teresa na New Faraja vilivyopo Mburahati jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo, amewashukuru wananchi na walipakodi kwani mchango wao unatoa furaha kwa watu wenye mahitaji maalumu ambao wanalelewa na kituo cha Mother Teresa.
Pia amewashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wa kituo hicho kwani kuna watoto wenye mazingira magumu lakini wanawatunza vizuri na wengine wametunzwa hapo na wanafanya kazi.
"Hawa wanasaidia nchi hawa pia ni walipakodi huwenda kisingekuwepo hiki kituo tusingepata watoto hawa amabao wanafanya kazi, tunawashukuru sana. Lakini sisi TRA tunarudisha kidogo kwa jamii, tulichokifanya hiki cha kutoa vyakula pamoja na vitu mbalimbali vya mahitaji mhimu ni sehemu ya TRA kuthamini kodi inayolipwa na wananchi lakini pia kurudisha kwa jamii hasa kwa watu wenye mahitaji Maalumu." Amesema Mwenda
"Tumeamua tuje tutoe kwa watu wenye mahitaji maalumu, hii ni kuonesha kwamba TRA sio tuu inakusanya kodi, pia inatoa kidogo kwa jamii."
Mwenda amesema kuwa Kama ambavyo TRA wamepeleka furaha kwa wenye mahitaji hivyo na watu wengine wenye uwezo walete furaha kwa watu hao.
Pia ameeleza kuwa kama kodi ikilipwa vizuri zaidi Serikali itatimiza majukumu yake lakini Kituo cha Mother Teresa wanachokifanya ni kusaidia jukumu la Serikali, lakini kadri uwezo wa Serikali unavyoongezeka inaweza kufanya majukumu hayo.
Aidha amewaomba wananchi kuendelea kuonyesha ushirikiano kwa Mamlaka hiyo ili waendelee kufanikisha ukusanyaji wa mapato nchini na kuisaidia serikali.
Kwa upande wa Mmoja ya wazee katika kituo hicho, ameipongeza TRA Kwa kuonyesha kuguswa na kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum na kuongeza kuwa msaada huo hautapotea na Mungu atalipa.
Mkurugenzi wa Kituo cha New Faraja, Zamda Idrisa Juma amewashukuru pia TRA Makao Mkuu kwa kuwapa sadaka ya Kristmasi na Mwaka Mpya.
"Tunashukuru msaada huu utatufaa sana kwa sikukuu na kwa vifaa vya shule kwaajili ya watoto shuleni ifikapo Januari Mwakani, tunashukuru sana Mwenyezi Mungu awabariki."