Na Linda Akyoo
Tume huru ya Taifa ya uchaguzi imeandaa utaratibu wa kuandikisha watanzania waliopo magereza wanaotumikia adhabu zisizozidi kifungo cha miezi 6 pamoja na Mahabusu kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Utaratibu huo ambao ni wa kwanza kutumika hapa nchini utawapa haki wafungwa hao na mahabusu kushiriki zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.
Taarifa hiyo imetolewa mjini Moshi na Mkurugenzi wa Huduma za kisheria wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi Seleman Mtibola wakati akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza kwa wadau wa uchaguzi.
Amesema tayari vituo 130 vimeshaainishwa Kati ya hivyo 10 viko visiwani Zanzibar wakati vituo 120 vipo Tanzania bara.
Katika hatua nyingine Tume huru ya Taifa ya uchaguzi imetangaza kuwaondoa wapiga kura 5494 kwenye daftari la kudumu wa wapiga kura kutokana na kukosa sifa za kuwa wapiga kura.
Mtibola amewataja baadhi ya watakaondolewa kwenye daftari Hilo ni pamoja na walioko kizuizini kwa Amri ya Raisi, waliofungwa gerezani kwa zaidi ya miezi 6 pamoja na wenye changamoto ya Afya ya akili.
Aidha Tume hiyo inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya milion tano laki tano themanini na sita elfu Mia nne thelathini na tatu ikiwa ni Sawa na 18.7% ya wapigakura wote wanaotarajiwa kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, Kulingana na taarifa hiyo miongoni mwa watakao andikishwa ni pamoja na waliotimiza umri wa miaka 18.
Pia wapiga kura 4369,531 wanatarajiwa kuboresha taarifa zao wakiwemo waliohama kutoka maeneo Yao ya awali na kwenda maeneo mengine.
Baadhi ya viongozi wa siasa waliodhuria Mkutano huo akiwemo Basili Lema kutoka chama cha demokrasia na Maendeo( CHADEMA) wamesema ni vyema elimu hii ikatolewe sio tu kwa viongozi Bali kwa wanachama pia ili kuwa na uelewa wa zoezi zima la uboreshaji wa Daftari hilo.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa tume ya huru ya uchaguzi Giveness Aswile ameto wito kwa Watanzania kujitokeza kuboresha taarifa zao wakati wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura 2024/2025.