MENDE ABAINISHA SABABU YA KUWANIA UNAIBU KATIBU MKUU TUCTA

 NA MWANDISHI WETU

EBENEZER Mende, ambaye ni mtumishi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), amebainisha kwamba ameamua kuwania nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi  Tanzania (TUCTA),  ili kuitendea haki karama yake ya uongozi na kuleta mabadilio yatakayokuwa na historia njema nchini.

Mende, anawania nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 14, 2024 jijini Arusha, kuziba nafasi ambayo imeachwa wazi na Cornel Magembe ambaye ameteuliwa kushika nafasi nyingine na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Nimeamua niitendee haki karama yangu ya uongozi kwa kujaza  nafasi  hiyo ili watanzania wenye matamanio ya kuona mabadiliko katika nyanja mbalimbali kuhusu utumishi wao zikifanyiwa kazi kama ambayo wanatarajia , Mungu atusaidie kufika siku hiyo.

“Pia Mungu awawezeshe wajumbe ambao ndio waidhinishaji wa mtu kuwa kiongozi, basi siku hiyo wanipigie kura mimi Ebenezer Mende, ili niiongoze nafasi hiyo na mabadiliko ya dhati yaweze kupatikana na ije kuwa historia njema ya nchi yetu na wafanyakazi wa Tanzania,” amesema.

Ameongeza kwamba anaamini akifanikiwa kupata nafasi hiyo, atajitahidi kuendana  na mazingira na matakwa ya wafanyakazi kwa kuwa na mabadiliko na kuacha historia ya mafanikio ya utofuti na neema, utofauti wa mazuri kati ya jana, leo na kesho iwe ni kubwa zaidi ya leo.

“Mungu atusaidie pamoja tuijenge Tanzania yetu,” amesema.

a.


Post a Comment

Previous Post Next Post