Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bw. Rodrick Mpogolo akizindua Programu Atamizi ya Ujasiriamali wa Mazingira Tanzania chini ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Biyoanuai kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja jijini Mbeya leo Novemba 06, 2024.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bw. Rodrick Mpogolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Atamizi ya Ujasiriamali wa Mazingira Tanzania chini ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Biyoanuai kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja jijini Mbeya leo Novemba 06, 2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Paul Deogratius akitoa neno la ukaribisho wakati wa uzinduzi wa Programu Atamizi ya Ujasiriamali wa Mazingira Tanzania chini ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Biyoanuai Luhemeja jijini Mbeya leo Novemba 06, 2024.
Mratibu wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Biyoanuai kutka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Damian Mapunda akitoa neno la utambulisho wakati wa uzinduzi wa Programu Atamizi ya Ujasiriamali wa Mazingira Tanzania chini ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Biyoanuai jijini Mbeya leo Novemba 06, 2024.
Washiriki mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa Programu Atamizi ya Ujasiriamali wa Mazingira Tanzania chini ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Biyoanuai jijini Mbeya leo Novemba 06, 2024.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bw. Rodrick Mpogolo akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wakati wa akizindua Programu Atamizi ya Ujasiriamali wa Mazingira Tanzania chini ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Biyoanuai jijini Mbeya leo Novemba 06, 2024.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bw. Rodrick Mpogolo akikagua mabanda ya wajasiriamali wakati wa uzinduzi wa Programu Atamizi ya Ujasiriamali wa Mazingira Tanzania chini ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Biyoanuai kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja jijini Mbeya leo Novemba 06, 2024.
……..
Tanzania imetajwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa mifumo-ikolojia ambapo takriban hekta millioni 48.1 za misitu ambayo ni wastani wa asilimia 51 ya eneo lote la nchi kavu.
Misitu hiyo ni makazi ya viumbe hai na baadhi yake ni vyanzo vya maji ambayo ina mchango mkubwa katika ustawi wa maisha na maendeleo ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii hapa nchini.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 06, 2024 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bw. Rodrick Mpogolo wakati wa uzinduzi wa Programu Atamizi ya Ujasiriamali wa Mazingira Tanzania chini ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Biyoanuai unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Bw. Mpgolo amesema kuwa pamoja na hayo pia Tanzania ni miongoni mwa nchi 12 duniani zenye utajiri mkubwa wa bayoanuai ikiwa na aina takribani 14,000 za mimea na wanyama wanaojulikanaAmeongeza kuwa ni miongoni mwa nchi 15 pekee duniani zenye idadi kubwa ya viumbe hai wanaopatikana Tanzania pekee hivyo.
kuiweka Tanzania kuwa katika kipaumbele cha uhifadhi wa mazingira duniani.Amesema programu iliyozinduliwa itachangia kuongeza uelewa na hamasa ya wadau wa urejeshaji ili kushiriki katika shughuli za urejeshaji kupitia ujasiriamali wa kimazingira pamoja na kubadilishana uzoefu.
Awali akitoa neno la ukaribisho, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Paul Deogratius amesema mradi huo ni muhimu katika kuchangia juhudi za kufikia malengo ya kitaifa ya urejeshaji wa mazingira hususan uoto wa asili ukitarajiwa kuchangia urejeshaji wa hekari 110,000 za maeneo kufikia mwaka 2025.
Amesema kwa kutambua nafasi ya sekta binafsi katika uhifadhi wa mazingira, mradi kupitia Shirika la Bridge for Billions (B4B) na Taasisi ya Ujasiriamali ya Anza unatekeleza Programu Atamizi ya Ujasiriamali wa Mazingira (The Restoration Factory), utekelezaji wake unahusisha uchaguzi wa miradi ya wajasiriamali wa mazingira, utoaji wa mafunzo ya kibiashara na usimamizi wa kitaalam kwa wajasiriamali pamoja na kuwezesha majadiliano na wawekezaji kwenye fursa za kibiashara za mazingira
Dkt. Paul ameongeza hadi sasa Programu ina wajasiriamali hai 42 kati ya 46 waliosajiliwa, ambapo asilimia 50 wapo moduli ya pili hadi ya moduli ya nne na asilimia 25 wapo moduli ya kwanza.
Ikumbukwe, mradi huu unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) na Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Mazingira (IUCN).
Mradi huu ni wa miaka mitano (2021-2025) na unafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF).Maeneo ya kipaumbele ya mradi ni Halmashauri za Wilaya saba zilizopo katika mabonde ya Ruaha Mkuu na Ziwa Rukwa, ambazo ni Iringa, Wanging’ombe, Mbarali, Mbeya, Sumbawanga, Mpimbwe na Tanganyika.
Tayari wajasiriamali wa mazingira 42 kati ya 46 ni hai na wameendelea na hatua mbalimbali za mafunzo tangu mwezi Agosti 2024 utekelezaji wa programu hii ilipoanza rasmi. Aidha, nimejulishwa kuwa Kati ya hao wajasiriamali wanaoendelea na mafunzo 28 ni wanaume na 14 ni wanawake.
Vilevile wajasirimali hao wamejikita katika shughuli za kilimo endelevu, ufugaji nyuki, uzalishaji wa bidhaa za mazao ya misitu, nishati safi, urejelezaji wa taka ngumu na uzalishaji wa mboji (Organic Fertilizers). Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza sana nyote mlioamua kuchangamkia fursa hii na naamini wadau wengi wataiga kutoka kwenu.