WADAU WAITWA KUTEMBELEA BANDA LA BRELA

 


NA MWANDISHI WETU

OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa ametoa wito kwa Watanzania na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi na kutembelea lao katika maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Wito huo ameutoa leo Julai 3, 2024 ndani ya viwanja vya maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea tuzo kutoka Rais, kwa kushika nafasi ya ushindi wa tatu wa jumla.

“Leo hii, tunashukuru kutokana na utendaji wetu tumefanikiwa kushika nafasi ya tatu kwa matokeo ya ujumla na kupewa tuzo ya Ngao na Mheshimiwa Rais, hii ni uthibitisho kuwa Brela tumetoka wapi na tunakwenda wapi .

“Hivyo banda letu limefanikiwa kuwa mshindi wa tatu kwa jumla ingawa mwaka jana tulifanikiwa kushima nafasi ya pili kwa taasisi zinazofanya kazi kama za kwetu, hivyo tunapoelekea tunataka tuone hiki ambacho tumepata leo katika maonesho ya haya yanahakisi katika utendaji wetu wa kila siku kama taasisi ya Serikali.

“Hivyo nitioe wito kwa wananchi na wadau wetu waje kwa wingi katika banda letu kupata huduma, kwani tunatoa huduma zote kama zile zinazotolewa ofisini kwetu na tutaendelea kuwepo hapa hadi Julai 15 mwaka huu,banda letu lipo karibu la lango kuu la kuingilia magari, waje kwa wingi watapata huduma stahiki na kwa haraka” amesema.


Post a Comment

Previous Post Next Post