Viongozi mbalimbali wa Serikali wametembelea Banda la MSD kwenye maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 June, 2024.
Miongoni mwa viongozi waliotembelea ni Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Mhe. Ridhiwani Kikwete (Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mhe. Simbachawene amesema anafurahishwa na namna MSD inavyotekeleza majukumu yake katika kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya “nimefurahishwa na namna MSD ilivyosambaza mashuka kwenye majimbo yetu ambayo yamesaidia katika utoaji wa huduma za afya”
Mhe. Simbachawene ameipongeza pia MSD kwa kupeleka haraka Jokofu la kuhifadhia miili Kituo cha Afya Kibakwe – Mpwapwa – Dodoma ambalo lilikuwa linahitajika kwa kiasi kikubwa.