WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA SADC WANAOHUSIKA NA MAZINGIRA, MALIASILI NA UTALII NGAZI YA MAKATIBU WAKUU KWA NJIA YA MTANDAO




Wizara ya Maliasili na Utalii leo Juni 20 2023 imeshiriki Mkutano wa SADC Ngazi ya Makatibu Wakuu  jijini Dodoma. 

Lengo la mkutano huo ni kufuatilia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika mikutano iliyopita ya wakuu wa nchi na serikali wa SADC, Baraza la Mawaziri la pamoja la SADC, na Mikutano ya Mawaziri wa kisekta wa SADC.

Nkutano huo umehudhuriwa na washiriki kutoka Nchi zote 16 za SADC.

Kwa upande wa Tanzania mkutano huo umehudhuriwa na Mwenyekiti ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt Switbert Mkama, Makamu Mwenyekiti ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki , Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Deusdedit Bwoyo, Mkurugenzi msaidizi Mazingira, Dkt.Thomas Bwana, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii,Bure Nassibu, Maafisa kutoka idara ya Mazingira (Ofisi ya Makamu wa Rais) na Maafisa kutoka idara za Sera na Mipango, Utalii, Misitu na Nyuki na Wanyamapori (Wizara ya Maliasili na Utalii).

Post a Comment

Previous Post Next Post