UTALII NI UKARIMU SIO VIBOMU KWA WAGENI-DKT. ABBASI

 

………………..

Leo Katibu Mkuu-Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amemwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Mohamed_mchengerwa kufunga semina ya waongoza utalii zaidi ya 1,200 iliyoratibiwa hiyo na Wizara na Tanzania National Parks jijini Arusha.

Amewataka na kuwakumbusha waongoza watalii (tour guides) kuwa wao ni taaluma muhimu sana katika kuwahudumia na kuwakirimu wageni na kuwakumbusha watafurahia matunda ya maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Royal tour tanzania iwapo watajiongeza, watajiimarisha na watatenda kazi kwa weledi badala ya kuwekeza katika “uzabizabina na ukiroho papo.”

“Ninyi ni waongoza utalii na sio waondosha watalii; fanyeni kazi kitaalamu na kwa ukarimu wa juu sana na sio kuwaongezea ‘stress’ watalii mara unaweka vibomu kwa kueleza shida zako mara nini, msingi wa huduma yenu kwa watalii ni ukarimu sio vibomu,” alisema Dkt. Abbasi, akieleza pia katika semina hiyo mafanikio lukuki katika mwaka
mmoja wa filamu ya Royal Tour.

Post a Comment

Previous Post Next Post