DKT. ABBASI :TAASISI ZA MALIASILI ZIJITOFAUTISHE

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kujitofautisha kwa kufanya kazi kwa weledi na maadili ili kuondoa dhana hasi dhidi ya Wizara hiyo aliyosema ni ya kimkakati kwa uchumi wa nchi.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Aprili 11, 2023, Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Taasisi za Makumbusho ya Taifa pamoja na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) ikiwa ni muendelezo wa vikao vyake vya kiutendaji na viongozi wa taasisi hizo za Wizara.

“Hizi ni zama za Royal Tour taasisi za Wizara hii zinatakiwa kujipambanua kwa namna za kipekee, kuonesha utofauti na kwanini taasisi yako ni muhimu kuliko nyingine ili viongozi wa juu waweze kuona mchango wako katika kukuza utalii nchini”. Alisema Dkt. Abbasi huku akiwataka viongozi hao kuongeza ubunifu katika kazi zao.

Katika vikao hivyo Katibu Mkuu ameendelea kusisitiza juu ya falsafa mbili zinazotumiwa na Wizara kwa sasa ambazo ni Uhifadhi (Conservation) na Kutangaza (Kujitangaza).

Post a Comment

Previous Post Next Post