WAUGUZI WA JKCI WATOA HUDUMA ZA UPIMAJI NA ELIMU YA MAGONJWA YA MOYO DODOMA

 


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rehema Bakari akimpima mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo shinikizo la damu wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayoenda sambamba na maonesho ya siku tatu ya huduma zinazotolewa na wauguzi yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adam Ndamayape akimweleza mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kuhusu ugonjwa wa shinikizo la juu la damu wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayoenda sambamba na maonesho ya siku tatu ya huduma zinazotolewa na wauguzi yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akitoa elimu ya dalili za shambulio la moyo pamoja na madhara yake kwa wanafunzi wa Uuguzi kutoka Chuo Kikuu cha St. John kilichopo jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayoenda sambamba na maonesho ya siku tatu ya huduma zinazotolewa na wauguzi yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini humo.

Wananchi waliofika katika Banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakipata huduma za upimaji na elimu ya magonjwa ya moyo wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayoenda sambamba na maonesho ya huduma zinazotolewa na wauguzi yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Picha na JKCI

Post a Comment

Previous Post Next Post