EAC WAJA NA MIKAKATI KUDHIBITI TAKA ZA KIELETRONIKI

 Na Karama Kenyunko Michuzi TV


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Manzingira (mbunge), Khamis Hamza Chilo amesema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna bora ya kuchakata, kusimamia na kuhifadhi taka zitokanazo na vifaa vya kielektroniki.

amesema kuwa taka hizo zimekuwa zikiathiri mazingira hivyo Tanzania kama moja ya nchi wanachama watahakikisha wanapunguza na kudhibiti ongezeko la taka hizo.

Akizungumza wakati akifunga mkutano wa tano wa Taasisi za Mawasiliano EAC (EACO), uliofanyika jana Dar es Salaam, Khamis, amesema katika warsha hiyo ya siku tatu nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamefikia maazimio mbali mbali kuhakikisha kila nchi inadhibiti taka za kielektroniki ambazo huchangia athari za kimazingira na kibinadamu.

Aidh, nchi hizo zipo katika hatua mbalimbali za kuandaa miongozo ya majukumu muhimu kwa kampuni zinazozalisha vifaa hivyo.

"Kila nchi wanachama wanatakiwa kuhakikisha wana sera, sheria na kanuni na miundombinu ya kuwezesha uchakataji wa taka hizo kwa kuzingatia ikolojia na bajeti ya kuwezesha ukusanyaji wa taka hizo kuwa stahimilivu kwani zipo sheria, taratibu na hatua ambazo wamechukua kwa ajili ya kudhibiti suala hilo.

Amesema kwa kufuata miongozo hiyo, tunaweza kupunguza au kuondosha kabisa tatizo na changamoto la taka za kieletroniki kwa sababu kila kukicha tunapokea electronics tofauti zikiwemo nzima, mbovu na mpya kwa ajili ya matumizi yetu kama binadamu.

Amesema Tanzania imesaini mikataba mbalimbali ya kimataifa ya kudhibiti taka za kielektroniki na kwamba elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi waweze kuelewa kuhusu utunzaji wa taka hizo.

"Tutaenda kuwaelimisha wananchi kwamba tunaweza tukasafirisha na tukapunguza, kuondosha lakini pia tutawaelimisha wananchi wetu namna bora ya kuweza kuzichakata, kusimamia na kuhifadhi taka kwasababu taka hizi tusipozithibiti ni tatizo ambalo mwisho wa siku linakwenda kuadhiri mazingira kwa ujumla na namna bora ya kuzuia kwakuwa Kwasasa hali sio mbaya sana," amesema chill.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa EACO, Dk Ally Simba amesema, kukua kwa teknolojia na maendeleo kunaongeza taka za kieletroniki hivyo ni lazima kuwa na mikakati ya kudhibiti tatizo hilo.

Dk Simba ameeleza kuwa nchi zote zina kamati za taka za kielektroniki kwa Tanzania kamati hiyo inasimamiwa na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakiwa na jukumu la kutoa elimu kuhusu taka hizo.

Amesema haishauriwi kukaa na taka za kielektroniki nyumbani, vile ambavyo havifanyi kazi tuvitoe kwa watu wanaopita mitaani na kukusanya taka hizo ili wazichakate.

Amesema, mkutano huu ni watano katika nchi za Afrika Mashariki na kwamba nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi waliwahi kuwa mwenyeji wa mkutano huo na mwaka 2024 mkutano kama huo utafanyika Sudan Kusini na lengo kubwa ni kuelimisha kuhusu namna ya kuhifadhi na kudhibiti taka za kielektroniki
Naye, Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Emmanuel Mannaseh mesema Tehama imeongeza faida nyingi kijamii na kiuchumi lakini pia imeongeza idadi kubwa ya taka za kielektroniki.

Amesema wamekubaliana kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya ukusanyaji, uchakataji na uteketezaji wa taka za kielektroniki kwa kutengeneza vifaa vya plastiki na madini kutumika kutengeneza vifaa vingine.

"Tutahakikisha tunajenga miundombinu ya usimamizi wa taka za kielektroniki, kuongeza uelewa na ustahimilivu wa taka hizi kwa utunzaji wa mazingira na ustawi wa watu wetu," alisisitiza Dk Mannaseh.

"Kongamano hili limekuwa chachu na limekuwa na idadi kubwa ya waliohudhuriwa kupitia njia ya kawaida na ya kimtandao kutoka Nchi wanachama wa nchi za afrika mashariki.
Mtendaji wa Taasisi ya Mawasiliano ya Afrika Mashariki (EACO) Dkt Ally Simba akizungumza wakati wa Ufungaji wa Mkutano uliondaliwa na EACO kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka nchi saba za Afrika Mashariki kujadiliana kwa pamoja namna ya kukabiliana na taka zinazotokana na vifaa vya kielektroniki. Mkutano huo umefungwa leo Machi 22,2023 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Chilo akizungumza wakati akifunga Mkutano uliondaliwa na EACO kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka nchi saba za Afrika Mashariki kujadiliana kwa pamoja namna ya kukabiliana na taka zinazotokana na vifaa vya kielektroniki. Mkutano huo umefungwa leo Machi 22,2023 kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post