DKT. ABBASI: TUKATANGAZE UTALII KWA VIWANGO VYA “ROYAL TOUR.”

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesisitiza kasi, ubunifu na mikakati katika utangazaji wa vivutio vya Utalii nchini huku akisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imeshaonesha njia kupizia filami ya “Tanzania; The Royal Tour.”

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Jumapili Machi 12, 2023, wakati wa Kikao cha Kimkakati na Maafisa Habari, Uhusiano na Masoko wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Amesema visheni ya Rais na Waziri mpya wa Utalii, Mohammed Mchengerwa, ni kuona kwba wakati ni sasa wa kuimarisha uhifadhi lakini haidi kuwekeza katika kutangaza utalii ili kuipatia Serikalo fedha zaidi za kigeni.

"Kwenye kipindi hiki cha Uongozi mtarajie msisitizo mkubwa kwenye eneo la Uhifadhi na Utangazaji Utalii. Lazima tutangaze Utalii wetu, na ninyi ndio nguzo kuu kwa utaalamu wenu. Hatutarajii mtu akikwamisha azma hii na siku uote tuwaze makubwa kwa viwango vya filami ya “Royal Tour.”

Sanjari na hayo, Dkt. Abbasi amewataka Maafisa hao kuwa wabunifu ili waweze kuitangaza nchi na waache kufanya kazi kwa mazoea.

"Tuangalie namna mpya ya kuitangaza Tanzania, ni lazima tuwe na mbinu mpya za kutangaza tulicho nacho" amesema Dkt. Abbas

Vilevile amewataka Maafisa hao kuwa na umoja ili kufikia dhamira pana ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza sekta ya utalii nchini.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizarani, Bw. John Mapepele alisisitiza: "Ninyi ndio nguzo ya Utangazaji utalii, Ninyi mpo katika hifadhi kazi yenu kuu imekuwa ni kuhifadhi na sasa kutangaza zaidi ndio tunachosubiri kukiona kutoka kwenu.”  

Post a Comment

Previous Post Next Post