BRELA YATOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA TWCC JIJINI DAR

 

Afisa Usajili Msaidizi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA), Bw. Bethod Bangahanoze akitoa Elimu ya Usajili wa Jina la Biashara kwa Vijana waliotembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye maonesho ya Wajasiriamali yaliyoandaliwa na TWCC katika viwanja vya Mlimani city Jijini Dar es Salaam leo tar.12,March,2023.

BRELA imepiga kambi kwenye maonesho hayo yaliyofanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 9 hadi leo tarehe 12, Machi, 2023, ambapo wananchi mbalimbali wametembelea kwenye Banda lao na kupata Elimu sambamba na kusajili majina ya biashara zao.

Aidha pamoja na mambo mengine, taasisi hiyo imekuwa ikitoa Vyeti na Leseni papo kwa hapo kwa wananchi waliosajili Biashara zao katika maonesho hayo.

Afisa Leseni wa BRELA Saada Kilabula (kushoto) akiwa na Afisa Usajili Msaidizi wa Taasisi hiyo Bw. Bethod Bangahanoze (wa pili kulia) wakizungumza na mwananchi aliyetembelea Banda la Taasisi hiyo kupata Elimu.

Maafisa wa BRELA wakiwa katika majukumu yao katika maonesho hayo. (Kushoto) , ni Afisa TEHAMA wa Taasisi hiyo Fadhili Mlosa, (katikati), ni Afisa Leseni  Saada Kilabula, na (kulia) ni, Afisa Usajili Msaidizi wa Taasisi hiyo Bw. Bethod Bangahanoze.

Picha ya pamoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post