WAZIRI MBARAWA AKAKUGUA MRADI WA UJENZI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO JIJINI DODOMA

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 22,2023 wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Msalato unaojengea jijini Dodoma.

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ,akikagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Msalato unaojengea jijini Dodoma ziara iliyofanyika leo Februari 22,2023.

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akimskiliza Meneja Mradi Makao Makuu kutoka Wakala wa Barabara (Tanroads),Mhandisi Kendrik Chawe wakati wa ziara ya waziri ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Msalato unaojengea jijini Dodoma leo Februari 22,2023.

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa,akizungumza na waandishi wa habari lep Februari 22,2023 wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Msalato unaojengea jijini Dodoma.

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimskiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jonathan Nzayikorera,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Msalato unaojengea jijini Dodoma ziara iliyofanyika leo Februari 22,2023 .

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jonathan Nzayikorera mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Msalato unaojengea jijini Dodoma ziara iliyofanyika leo Februari 22,2023 .

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa,ameridhishwa na Mwenendo wa Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato huku akimtaka Mkandarasi kuongeza kasi ili kukamilisha mradi huo wa kimkakati kwa muda uliopangwa kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Hayo ameyasema leo Februari 22,2023 jijini Dodoma mara baada ya kutembelea na kukagua mradi huo ambapo amesema kuwa kazi ya ujenzi wa uwanja huo inaendelea vizuri.

“Leo tumekuja kutembelea mradi na kuona kazi inavyoendelea, tumeona maendeleo ni mazuri na kazi inakwenda kama inavyotakiwa tunaimani kuwa mkandarasi ataongeza kasi zaidi ili ukamilike kwa muda uliopangwa kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla”amesema Prof.Mbarawa

Aidha amesema kuwa sehemu ya kwanza ya Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato inayohusisha ujenzi wa eneo la ndege kuruka na kutua umefikia asilimia 13.

Prof. Mbarawa amesema kuwa sehemu ya kwanza ya ujenzi huu inahusisha ujenzi wa eneo la ndege kutua na kuruka ambalo lina urefu wa km 3.6 na sehemu ya pili inahusisha ujenzi wa majengo ikiwemo jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, ofisi, jengo la zima moto pamoja na miundombinu mingine.

Amesema kuwa sehemu ya kwanza ya ujenzi wa eneo la ndege kutua na kuruka linagharimu kiasi cha bilioni 164 na sehemu ya pili inayohusisha ujenzi wa miundombinu ya majengo utagharimu kiasi cha bilioni 194.4.

“Sehemu ya kwanza ya ujenzi inayohusisha ujenzi wa eneo la ndege kutua na kuruka mpaka sasa imefikia asilimia 13 na kwa upande wa sehemu ya pili ya ujenzi wa majengo na miundombinu mingine bado mkandarasi yuko katika hatua ya maandalizi kama mlivyoona” amesema Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jonathan Nzayikorera amesema kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika inamshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake imara na maono aliyonayo katika mradi wa ujenzi huo.

“Nitaenda kusema nilichokiona, maendeleo ni mazuri sana, nimefurahishwa na kasi ya ujenzi inavyoenda lakini niwaombe makandarasi kuhakikisha kuwa wanatekeleza na kufanya kazi kwa wakati ili mradi huu ukamilike ndani ya wakati” amesema Bw.Nzayikorera

Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila amesema kuwa sehemu ya kwanza ya mradi huo imefikia asilimia 13 kwa kuwa mkataba wa ujenzi wake ulisainiwa mapema mwaka 2021 wakati ujenzi wa sehemu ya pili ya ujenzi wa majengo ulisainiwa mwaka 2022.

“Wakati Rais Dk. Samia akiweka jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa ujenzi huu aliwataka makandarasi wa ujenzi wa mradi huu kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kuwa mradi unakamilika mapema iwezekanavyo” amesema

“Uwanja huu ni uwanja mkubwa na wa kimataifa, ukikamilika utaleta mapinduzi makubwa Dodoma kwa kuwa ndege kubwa zilizokuwa zinashindwa kutua zitatua sasa na hata wageni wakubwa wanaokuja kuonana na rais badala ya kutua KIA au JNIA watatua Dodoma moja kwa moja” ameongeza Mhandisi Mativila

Post a Comment

Previous Post Next Post