MTENDAJI MKUU TEMESA ATOA MWITO TAASISI ZA UMMA NA SERIKALI ZINANAZODAIWA

 Na. Alfred S. Mgweno (TEMESA)


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro N.
Kilahala ametoa wito kwa Taasisi za Umma na Serikali zinazodaiwa na Wakala huo
baada ya kupatiwa huduma za matengenezo ya magari, mitambo, huduma za
ufundi, umeme na elektroniki, kuilipa TEMESA madeni inayowadai ili Wakala huo
uweze utekeleza majukumu yake kwa ufanisi.


Kilahala ametoa wito huo Tarehe 03 Februari, 2023, alipokuwa akizungumza katikakikao cha Wadau wanaopatiwa huduma na TEMESA Mkoa wa Dodoma, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ulioko
Makole mjini Dodoma ambapo kimehudhuriwa na maafisa mbalimbali
wanaowakilisha Taasisi za Umma wakiwemo maafisa usafirishaji, maafisa kutoka
Serikali kuu, Wizara mbalimbali, wawakilishi wa karakana teule zinazofanya kazi kwa pamoja na TEMESA pamoja na wazabuni wanaosambaza vipuri na vitendea kazimbalimbali kwa Wakala huo.


Mtendaji Mkuu amesema, anafahamu changamoto ambazo wanakutana nazo
kwenye Taasisi na Wizara zao ikiwemo kutokutosha kwa mgawanyo wa fedha za
maendeleo lakini akawataka kulipa uzito suala la kulipa madeni yao kwa TEMESA
kwakuwa ili wao (Taasisi) waweze kufika kwa mwananchi kumpatia huduma
wanahitaji kuwa na usafiri wa uhakika na ili wawe na usafiri wa uhakika, TEMESA
inahitaji kuwa na uhakika wa kupata vipuri vya kuwatengenezea magari ya Taasisi
zao kwahiyo kwa kutowalipa TEMESA kwa wakati kutasababisha ishindwe
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwani Wakala pia utakosa vipuri vya
kuwatengenezea magari ya Taasisi zao na hivyo kurudisha nyuma maendeleo.


‘’Wito wangu mkubwa sana kwenye eneo la Matengenezo na Huduma za Ufundi, nikwa wateja wetu, tunawaita washitiri, washitiri wetu tunawaomba chondechonde,suala la kutulipa mlitilie mkazo, kwasababu msipotulipa nyie huu mzunguko wapembetatu tunaousema unakuwa hauna maana na unakufa, na ukifa sio faidakwenu, sio faida kwetu (Wakala), sio faida kwa wazabuni, lakini sio faida kwa nchi,kwahiyo tujitahidi sana kadiri ya uwezo wetu, najua changamoto ni nyingi lakini tulipe uzito unaostahili suala hili, tulitilie mkazo sana suala hili na tujitahidi kadiri ya uwezo wetu.

’’ Amesema Mtendaji Mkuu na kuongeza kuwa TEMESA ipo kwa ajili ya
kuhudumia wananchi na hivyo kama wakiamua kuzuia magari ambayo Taasisi zakehazilipi madeni yao maana yake watasababisha mwananchi akose huduma
anayostahili kuipata na hivyo Wakala unaweka uzalendo mbele ili kuhakikisha
mwananchi anapata huduma anayoistahili na hivyo Taasisi hizo zinapaswa kuweka
uzalendo mbele kwa kulipa kwa wakati madeni yao.


Akizungumza kuhusu madeni ambayo Wakala unadaiwa na wazabuni ambao
waliikopesha vipuri miaka ya nyuma, Kilahala amesema TEMESA haipuuzii na wala
haijasahau kama inadaiwa na wazabuni hao, na ina wajibu wa kuwalipa. Mtendaji
Mkuu amesema kuwa ipo timu ambayo imekwishaundwa kwa ajili ya kuyahakiki
madeni hayo ikiwashirikisha wataalamu kutoka TEMESA, Wizara ya Ujenzi, MkaguziMkuu wa Ndani wa Serikali, wataaalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipangopamoja na wataalamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

‘’Niwaombe tuwe wavumilivu na tuzidi kuamini kwamba hakuna mtu ambaye
atadhulumiwa,mmemskia nyie wenyewe Mhe. Rais mara kwa mara anaweka wazi
kwamba yeye hataki kuendesha Serikali ya dhulma, hataki kuona mtu anapoteza
haki yake kwasababu amefanya kazi na Serikali, na sisi ni watekelezaji wa yale
maagizo kwa hiyo msimamo na dhati ya Serikali ni kuhakikisha kwamba kila
mwenye haki yake ataipata, kwahiyo niwatoe hofu’’ Alimaliza Mtendaji Mkuu.


Naye Meneja wa TEMESA Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Greyson Maleko,
akizungumza katika kikao hicho, amewashukuru wadau wote waliohudhuria kikao
hicho zikiwemo Taasisi ambazo hazikuvuka na madeni kwa mwaka uliopita.


Mhandisi Maleko alimuongoza Mtendaji Mkuu kutoa tuzo ya kutambua mchango kwaMashirika na Taasisi za Umma na Serikali kuu ambazo zimekuwa na mwendelezowa kulipa madai wanayodaiwa na ofisi za Wakala huo kwa Mkoa wa Dodoma kwawakati bila kuchelewa. Kilahala amezishukuru Taasisi hizo kwa kuendelea kulipamadeni yao kwa wakati na kuwaahidi kuwa Wakala utaendelea kuwapatia hudumailiyo bora wakati wote na kwa ufanisi mkubwa ili na wao waweze kutekelezamajukumu yao kwa wakati na kwa ufanisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post