Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Pindi Chana (Kulia) akiteta jambo na Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TNBC), Dkt. Godwill Wanga ( Katikati) kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya misitu waliokutana jijini Arusha kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki kutoka wizara ya maliasili na Utalii Bw. Deosdedit Bwoyo.
Na Mwandishi wetu, Arusha
WADAU wa sekta ya utalii na misitu wamezipongeza hatua za serikali ikiwa ni pamoja na kudumisha utamaduni wa kukutanisha wajumbe wa sekta binafsi na sekta ya umma katika kujadili changamoto zinazokabili sekta za utalii na misitu.
Wadua hao walihudhuria mikutano ya utalii and misitu iliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TNBC)
Wakizungumza kwa nyakazi tofauti wadau wamesema Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendeleza utamadini huo na kwamba imeonyesha dhamira ya kutatua na kuondoa vikwazo vyote vinavyokabili sekta hizo .
Mikutano kama hii ya kisekta imekuwa chachu kwani inatukutanisha wadau mbalimbali kujadii changamoto na kutoa mapendekezo ya kukuza sekta hizi, walielezana na pia kumpongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Pindi Chana, kwa kuhudhuria na kuchangia mawazo katika mikutano hii.
Mwakilishi wa Zanzibar Association of Tour Operators (ZATO), Bw. Hassan Ali Mzee, alipongeza mikutano hiyo inayoandaliwa na TNBC na kusema imewapa wadau uwanja mpana wa kutoa kero zao katika sekta hizo na imechochea ari kuendelea kuwekeza katika sekta hizo.
“TNBC amekuwa akituunganisha na serikali katika kujadili namna tutakavyokuza na kuendeleza sekta za miliasili na utalii. Sekta hizi ni muhimu katika kuinua pato la taifa, kuingiza fedha ya kigeni na kutengeneza ajira kwa vijana,” alisema Bw. Mzee
Bw. Benedict Minja, kutoka Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA). alipongeza azimio la kuwa na wiki ya maonyesho maalum ya bidhaa za misitu na kusema kwamba maonyesho hayo yatawafanya wananchi kutambua ubora wa bidhaa za mazao ya misitu zinazotengezwa Tanzania.
“Wiki hii ya maonyesho maalum itakayofanyika kila mwaka tunatarajia itaonyesha bidhaa bora na kuonyesha ustadi wa Watanzania katika kutengeneza bidhaa zinazotokana na misitu. Inaelekea Watanzania bado tuna kasumba ya kuthamini mno bidhaa kutoka nje,” alisema Bw. Minja. Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma.
Akifunga mkutano huo mwishoni mwa juma hapa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Pindi Chana, alisema Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezifungulia fursa sekta za maliasili na utalii kupitia Filamu ya Royal Tour, Filamu hiyo imeongeza idadi ya wawekezaji katika sekta ya utalii nchini, alisema waziri.
Alisema kuna haja ya kuangalia upya namna yakuongeza uwekezaji katika huduma za malazi kama vile hoteli na kambi za kitalii, migahawa, usafirishaji watalii, na uwindaji wa kitalii.
Aidha alitoa wito kwa wadau wote katika biashara za utalii nchini kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia biashara za utalii nchini ili utoaji huduma kwa watalii uwe bora, salama na wakuvutia.
Katibu Mtendaji waTNBC, Dkt. Godwill Wanga, alisema moja kati ya maazimio ya mikutano hiyo linahimiza ujoaji wa mafunzo kwa wadau wote wanaohudumia watalii wakiwemo wapagazi, waongozaji na watoa huduma na wahifadhi wa milima. Azimio lingine linahusu kuinua ujuzi katika uzimaji wa moto ili kuondoa misukasuko endapo janga la moto litatokea katika mbuga na hifadhi za utalii, alisema Dkt. Wanga