UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA PARIS,BODI YA UTALII TANZANIA WASHIRIKI MAONESHO YA 43 YA KIMATAIFA YA UTALII

 UBALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa  Paris, kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na wadau wengine wa Sekta ya Utalii nchini  wakishiriki  Maonyeshi ya 43 ya Kimataifa ya Utalii (FITUR), mjini Madrid, Uhispania


Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya utalii nchini, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Paris, unaowakilisha pia Falme ya Uhispania na Shirika la Umoja wa Mataifa  la Utalii Duniani (UNWTO), lenye makao yake makuu mjini Madrid, Uhispania na kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), umehamasisha na kushiriki katika Maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Utalii (43rd International Tourism Fair - FITUR), yaliyoanza tarehe 18   hadi 22 Januari 2023, mjini Madrid.

Maonyesho hayo ya kila mwaka ambayo hukutanisha wadau wa utalii kutoka nchi mbali mbali duniani yalijumuisha pia ushiriki wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori Ngorongoro (NCAA) na wadau wa utalii (Tour Operators) ambao kwa pamoja walifanya banda la Tanzania kuwa kivutio katika maonyesho hayo yanayohudhuriwa kwa wingi.

Wakatu wa ufunguzi tarehe 18 Januari 2023, uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa  la Utalii (UNWTO), ulifika bandani hapo na kuisifu Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika kuutangaza utalii nchini.
Washiriki wa maonyesho ya Utalii ya Fitur kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika wa Shirika la Umoja wa  mataifa la Utalii Duniani (UNWTO),  Bi. Elcia Grandcourt ( mwenye suti katikati) akiwa na ujumbe wake wa UNWTO walipotembelea banda la Tanzania wakati wa maonyesho ya Fitur mjini Madrid.

Post a Comment

Previous Post Next Post