Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara *Dkt.Hashil Abdalah* amekutana na timu ya Manejimenti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) ikiwa ni utaratibu wake wa kukutana na taasisi zilizopo chini ya Wizara.
Dkt.Hashil ameitaka menejimenti kuhakikisha Sekta ya Biashara nchini inakuwa kwa kasi na kuleta matokeo chanya kwa Taasisi ,Wizara na taifa kwa ujumla.
Dkt.Hashil amesema kuwa ,Tantrade imekuwa taasisi yake ya kwanza kukutana nayo kutokana na majukumu na umuhimu wake kwa Taifa katika kuendeleza Biashara za ndani na nje ya nchi.
Aidha amesisitiza uwajibikaji na uadilifu kwa watumishi wote ili kuhakikisha Jamii inapata Huduma Bora na kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bi.Latifa Khamis amemshukuru Katibu Mkuu kwa
Kuitembelea taasisi na ameahidi kuendelea kusimamia majukumu ya taasisi Kwa ufanisi.