Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amefurahishwa na Tamasha la Bata Msituni ambalo liliandaliwa na Chinobychino Travel kwa kushikiriana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo amesema kuwa matamasha kama hayo yanatakiwa kufanyika Tanzania nzima ili watu wafurahi.
Mhe. Mchengerwa alisema hayo wakati akizindua Tamasha hilo lililofanyika Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Pugukazimzumbwi Safu ya Vikindu uliochini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Alisema Watanzania wanafanya kazi sana hivyo baada ya majukumu yao ni muhimu kupumzika na hivyo matamasha kama hayo ni muhimu sana.
Aidha, Mhe. Mchengerwa aliwapongeza waandaaji kwa kuwa na ubunifu huo mkubwa na kuwasihi waendelee kuandaa matamasha hayo zaidi huku wakiwahusisha mamlaka husika.
Mgeni Rasmi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi ambapo alipongeza ubunifu huo na kusisitiza kuwa matamasha kama haya yanatakiwa kufanyika Tanzania Nzima, alizungumza hayo wakati wa Tamasha kubwa la Bata Msituni Lililofanyika katika Msitu wa Vikindu Safu ya Pugu Kazimzumbwi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir akitoa salamu za shukurani kwa muitikio Mkubwa wa watu waliofika katika Tamasha la Bata Msituni lililofanyika katika Msitu wa Vikindu safu ya Pugu Kazimzumbwi uliochini ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)
Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa akitoa burudani ya nguvu huku watu wakifurahia wakati wa Tamasha kubwa la Bata Msituni ambalo lilifanyika katika msitu wa Vikindu Safu ya Pugu Kazimzumbwi ambao Msitu huo upo chini ya Wakala wa Misitu Tanzania TFS
Wanamwita Chui, Rayvan hapa akiwa anakiwasha wakati wa Tamasha la Bata Msituni ndani ya Msitu wa Pugu Kazimzumbwi Safu ya Vikindu Mkuranga , Msitu huo upo chini ya wakala wa Misitu Tanzania TFS
Ukisikia piga kigoma mpaka unaamka ni hiki sasa Mgeni Rasmi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa, hapa akaona hapana ikabidi aungane na wanabata msituni kufurahia Tamasha kubwa la Bata Msituni huku Kigoma kikiendelea. (Picha na Fredy Njeje Mdau wa Utalii)